Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui Amekutana na Kuzungumza na Ujumbe wa Wockhardt Hospital.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi  zawadi maalum mjumbe kutoka Hospital ya Wockhardt ya Nchini India Somnath Shetty,alipofika Ofisini  kwake kujitambulisha.
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii , Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui  akipokea zawadi maalum kutoka kwa mjumbe wa Hospital ya Wockhardt  ya Nchini India Somnath Shetty, alipofika Ofisini kwake kujitbulisha .
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui afanya mazungumzo   na ujumbe kutoka Hospital ya Wockhardt ya Nchini India yenye lengo   la kuimarisha sekta ya Afya Zanzibar ,huko Ofisini kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar. 
Picha na Fauzi Mussa --Maelezo Zanzibar. 

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar .01/03/2022.

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe.Nassor Ahmed  Mazrui amesema madaktari  bingwa kutoka India wanatarajia kuweka kambi Zanzibar kwa lengo la kuimarisha sekta ya afya nchini. 

 

Akiyasema hayo huko Ofisini kwake Mnazi Mmoja wakati wa hafla fupi ya ujumbe kutoka India uliyofuatana na Mkuu wa Biashara za Kimataifa Somnath Shetty kutoka wockhardt Hospitals LTD .

 

Alisema ujumbe huo unatarajia kushirikiana na Wizara ya Afya kwa kuimarisha huduma za afya kwa jamii pamoja na utoaji huduma za kesi za upasuaji kwa wagonjwa mbali mbali .

 

Aidha alisema kesi mbali mbali wanatarajia kuzishughulikia zikiwemo kesi  za wagonjwa wanaohitaji kusafirishwa nje ya nchi.

 

Alifahamisha wajumbe hao wanatarajia kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kupitia sekta ya afya kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu bora   kwa wananchi wake .

 

Waziri huyo alifurahishwa na ujumbe huo wenye lengo la kuisaidia Zanzibar katika utoaji wa huduma za afya na kueleza fursa hiyo itasaidia kuwajengea uwezo pamoja na ujuzi wa kiutendaji kupitia kwa Madaktari Bingwa kutoka India katika hospitali za Mkoa na Wilaya

 

“Serikali  imejenga hospitali nyingi za Wilaya na Mikoa hivyo ni fursa pekee ya kupata wataalamu hao ambao watasaidia kutoa ujuzi kwa wafanyakazi pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi,”alisema Waziri  .

 

Nae Mkuu wa Biashara Kimataifa Somnath Shetty kutoka wockhardt Hospitals LTD amesema lengo la ujio wake ni kuleta mashirikiano ya pamoja katika kuwapatia huduma bora wananchi wa Zanzibar .

 

Amesema azma yao hiyo ni kuweka  kambi ya Madaktari bingwa  hapa Zanzibar kwa kutoa huruma mbali mbali za kiafya ikiwemo za upasuaji wagonjwa wenye kesi ambazo zinahitaji kusafirishwa nje ya nchi .

 

Akitoa Rai kwa wananchi wa Zanzibar aliwataka   kukata bima ya afya  ya kimataifa ili kuwasaidia  kupatiwa huduma ya afya ya nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.