Habari za Punde

CHANDE: Liwale Kamilisheni Taratibu za Maombi ya Fedha za Mradi wa Kimkakati.

 

Na.Peter Haule na Saidina Msangi, WFM, Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb, ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Liwale kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kukamilisha taratibu za maombi ya fedha za kutekeleza mradi wa Stendi ya kisasa ya Liwale na kuwasilisha Wizara ya Fedha na Mipango.

Rai hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Liwale, Mhe. Zuberi Mohamedi Kuchauka, aliyetaka kujua mpango wa Serikali kuirejeshea Halmashauri ya Liwale fedha za kutekeleza miradi ya kimkakati ilizozirejesha Hazina.

“Halmashauri ya Wilaya ya Liwale imetengewa shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa stendi hiyo katika mwaka 2021/22, nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa kutokana na umuhimu wake”, alieleza Mhe. Chande.

Alisema kuwa ujenzi wa stendi ya Kisasa ya Liwale mkoani Lindi ni moja kati ya miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato kwa Halmashauri ambapo mwaka 2018 Serikali iliingia mkataba na Halmashauri ya Liwale kutekeleza mradi huo kwa gharama ya shilingi bilioni 1.2.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.