KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi amewasili mkoani Manyara kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo amepokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiongozwa na Katibu wa Chama hicho mkoa Naomi Kapambala.
Shaka ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Manyara baada ya kuwasili na kupokelewa, atapokea taarifa ya @ccmtanzania Mkoa hasa inayoelezea hali ya Chama pamoja na utekelezaji wa Ilani ya chama hicho,pia atapokea taarifa ya Serikali Mkoa pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo, ambapo baadhi ya miradi imekamilika na mingine utekelezaji unaendelea. @ccmtanzania @daniel_godfrey_chongolo @shakazulu36 #babati #manyara
No comments:
Post a Comment