Habari za Punde

Moto wateketeza Bweni la Wanafunzi wa Skuli ya Ufundi Kengeja Pemba na Kusababisha Hasara Kubwa Mali za Wanafunzi wa Skuli hiyo.

Wanafunzi wa Skuli ya Ufundi Kengeja wakiwa katika viwanja
vya Skuli hiyo baada ya mabweni yao kuteketea kwa Moto na kupoteaza vifaa vyao mbalimbali wakiwa na baadhi ya vifaa walivyowahi kuvitowa wakati wa ajali hiyo iliyotokea jana na kuteketea kila kiliomo ndani.wanafunzi 96 waathiriwa na Moto huo, wanafunzi 44 wa kike watakiwa kubaki nyumbani siku mbili.

Sehemu ya mabaki ya vifaa na vitu vya Wanafunzi wa Skuli ya Ufundi Kengeja vilivyoteketea kwa moto wakati wa ajali hiyo iliyotokea katika moja wa Bweni la Wanafunzi wa skuli hiyo.

Na Hassan Msellem, Pemba                                                                                                                        

Wanafunzi 96 wa Skuli ya Ufundi Kengeja wamelazimika kusitisha masomo Kwa Kipindi Cha siku mbili baada ya vyumba vitatu vya dahalia walivyokuwa wakivitumia Skulini hapo kuungua Kwa Moto na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo Ndani ikiwemo Nguo za wanafunzi hao, vitabu, madaftari pamoja na mabegi jambo ambalo limepelekea wanafunzi 44 kati hao ambao ni wanafunzi wa kike kuruhusiwa kurudi nyumbani Kwa siku mbili ili kuipisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar kufikiria mbinu mbadala ya kukabiliana na athari zilizopatikana kutokana na tukio Hilo la Moto ili wanafunzi hao waweze kuendelea na masomo.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi huko katika Skuli ya Ufundi Kengeja Afisa mdhamin kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mohammed Nassor Salim amesema kutokana na athari zilizopatikana kutokana na Moto huo Wizara imelazimika kutoa pendekezo la kuwataka wanafunzi wote wakike ambao wameathiriwa na Moto huo kisalia nyumbani Kwa kipindi Cha siku mbili ili kuipisha Wizara kufanya tathmini ya namna ya kuandaa mazingira mbadala ili wanafunzi hao waweze kuendelea na masomo Kwa Amani.

Nae kaimu Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Abdu Ali Haji amesema tukio limewaathiri Kwa kiasi kikubwa kwani wanafunzi walikuwa katika Hali ya Maandalizi ya mitahani Yao ya kidato Cha nne ikizingatiwa kuwa Skuli ni miongoni Mwa Skuli za Serikali zinazoangaziwa kufanya Vizuri katika mitihani ya kitaifa.

Nao Baadhi wanafunzi walioathirika na tukio Hilo wameiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Kwakushirikiana na wadau wengine kubuni njia za haraka zakuweza kuandaa mazingira rafiki ya kuendelea na masomo ili tukio Hilo lisiwe ndio Chanzo Cha wanafunzi kufeli katika mitihani Yao kikanda na kitaifa.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.