Habari za Punde

Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD FDD Atembelea Shule ya Uongozi Kibaha.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo pamoja Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Mhe. Ndikuriyo Reverien (kushoto) na wajumbe wengine wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Chama Cha Mapinduzi Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Mganwa Nzota (kulia) walipotembelea Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo (kulia)akimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Mhe. Ndikuriyo Reverien mara baada ya kumaliza ziara ya kuitembelea Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, wengine pichani ni Balozi wa Burundi Nchini Tanzania Mhe. Gervas Abayeho na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (kushoto).Katibu Mkuu wa Chama Cha CNDD-FDD cha Burundi Mhe. Ndikuriyo Reverien pamoja na ujumbe wake wakiongozwa na mwenyeji wake, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo leo tarehe 18, Mei 2022 wametembelea Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Mhe. Ndikuriyo Reverien (kushoto) kwenye moja ya madarasa ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo pamoja Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha Burundi Mhe. Ndikuriyo Reverien (kushoto) na wajumbe wengine wakipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Chama Cha Mapinduzi Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndugu Mganwa Nzota (kulia) kwenye moja ya madarasa ya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.