Habari za Punde

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Azungumza na Uongozi wa ZATU na WEMA.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Othman Masoud Othman, leo Mei 25,2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chama cha Walimu Zanzibar (ZATU) pamoja na Viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar (WEMA).

Kikao hicho ambacho ni muendelezo wa ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais iliyoanza mapema mwezi Machi mwaka huu katika sekta ya Elimu Zanzibar, yenye lengo la kutambua changamoto na kuzitafutia ufumbuzi wake kimefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar iliyopo Migombani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akimsikiliza  Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Sera na Utafiti wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mwal. Khalid Masoud Waziri, katika kikao cha kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili Sekta ya Elimu Zanzibar.Kikao kilichofanyika katika ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Migombani Zanzibar Mei 25,2022.
 (Picha na OMKR Zanzibar)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.