Habari za Punde

Mhe Hemed asikitishwa na vitendo vya udhalilishaji watoto


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ameeleza kusikitishwa kwake kwa baadhi ya wazazi na walezi kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji watoto wao waliowazaa.

Alhajj Hemed ameelza hayo wakati akiwasalimia waumini wa Masjid Munawwar Chumbuni alipojumuika nao katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

Amesema matendo hayo yamefikia hatua ya kusikitisha na kueleza kuwa Serikali inaendelea kupiga vita matendo hayo ambapo baadhi ya wazazi na nwalezi bado wanaendelea na matendo hayo maovu yenye kurejesha maendeleo nyuma.

Hemed ameeleza kuwa vitendo vya udhalilishaji kwa watoto vinaathiri  watoto kiakili,kimwili pamona na kifikra na kupelekea  Serikali kukosa nguvu kazi ya Taifa kutokana na watoto hao kuathirika kisaikolojia.

Pia Makamu wa Pili wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Dkt Mwinyi itahakikisha inapambana na wale wote wanaoendelea kufanya matendo ya udhalilishaji kwa wanawake na watoto kwa kutoa adhabu kali dhidi ya wafanyaji wa vitendo hivyo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameendelea kuwaasa waumini na wananchi kwa ujumla kuendeleza matendo mema ikiwemo kusaidiana na kuhurumiana jambo ambalo linaongeza mapenzi na huruma baina ya Wananchi.

Sambamba na hayo Alhajj Hemed ameeleza kuwa matendo mema katika jamii yanaondoa Chuki na husda baina ya wananchi kwa kuacha tofauti zao na kushikamana kwa pamoja katika kujenga jamii iliyo bora.

 

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameomba wananchi kuendelea kuiombea Dua Nchi ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na viongozi kwa kuwaletea maendeleo wananchi wake.

 

Akitoka Khutba katika Ibada hiyo  Ustadh Suleiman Ame Usi amewausia waumini kuutumia vyema muda kwa kufanya Ibada na yote yanayoridhiwa  katika Sheria ili kupata Radhi za Allah Mtukufu.

 

Ameeleza kuwa ni hasara kubwa kwa Muumuni aliebarikiwa Umri na kutoutumia vyema badala yake kufanya maasi ambayo yamewekewa adhabu kali siku ya Hisabu yakiwemo yale ya udhalilishaji

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.