Waziri wa Utali na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Siman Mohammed Said akizungumza na Mwenyekiti wa wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Ndg.Rahim Bhaloo akiwa na Watendaji wa Benki ya NMB baada ya kumaliza mkutano wao wa NMB Toursim Gala uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Al Bahr Mbweni Unguja Jijini Zanzibar.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Benki ya NMB na Viongozi wa Kamisheni ya Utaliui na Wadau wa Utalii Zanzibar. baada ya kumalizika kwa mkutano na Wadau wa Utalii Zanzibar na Uongozi wa NMB uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madinat Bahr Mbweni Unguja Jijini Zanzibar.
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe.Simai Mohammed Said ameipongeza Benki ya NMB kwa uwekezaji wao wa shilingi Bilioni 100 ambazo zitatumika kuwakopoesha wadau katika sekta ya utalii Zanzibar.
Akizungumza katika hafla ya NMB Toursim Gala iliyofanyika katika hoteli ya Madinatul Bahr Mhe.Simai ameongeza kwa kushauri kwamba mikopo hiyo iende sambamba na kuwawezesha (Capacity Building) ili uwekezaji huo ili mikopo hiyo iendane na malengo.
Aidha aliushauri uongozi wa benki hiyo kuanza kuwajumuisha wadau wa sekta binafsi kutoka Zanzibar katika bodi zao wa wakurugenzi ili kusaidia kuwa karibu na wateja kutoka sekta tofauti.
Alizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi,Meneja wa kitengo cha ukaguzi wa ndani cha NBM (Internal Auditor) Benedict Baragomwa amesema kwamba Benki ya NMB inathamini jitihada za serikali katika kuleta maendeleo katika sekta hii hivyo basi na wao wamekuja na huduma tofauti zitakazomrahisishia mdau pamoja na kuendeleza uchumi kwa kupitia sekta hii. Huduma hizo ni kama kuongeza ATM katika mikoa ya Kaskazini na Kusini,Kuanzisha mfumo wa Bima pamoja na kadi maalumu itakayowanufaisha watembeza watalii ambao wamesajiliwa(ZATO Cards)
Nae Mwenyekiti wa ZATI ambae pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Bw.Rahim Bhaloo ameishukuru Benki hiyo huku akishauri huduma hizi zizidi kuendelea na kuangalia soko kwa upande wa Pemba.
No comments:
Post a Comment