Habari za Punde

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Mchengerwa Awakabidhi Kombe la UEFA Mashabika wa Timu ya Real Madrid Tanzania.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Tanzania .Mhe, Mohamed Mchengerwa  akiwakabidhi Kombe la Ubingwa Mashabiki wa Timu ya Real Madrid Nchini Tanzania, baada ya Timu yao kuibuka Bingwa mwaka huu baada ya kuifunga Timu ya Liverpool katika mchezo wa fainali ya Kombe la Uefa. 
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  akizungumza kabla ya kukabidhi Kombe hilo

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amewakabidhi kombe la UEFA mashabiki wa timu ya Real Madrid baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa usiku wa kuamkia leo huku akisisitiza kuwa  Wizara yake itaendelea kuwa bunifu kwenye sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuwapa furaha watanzania.

Mhe. Mchengerwa amesema hayo kwa wapenzi soka  katikati ya Daraja  la Tanzanite jijini Dar es Salaam kwenye tukio maalum la kuangalia mubashara fainali za UEFA lililoratibiwa na kampuni ya kinywaji cha  Heineken kwa  kushirikiana na Wizara  ya Utamaduni, Sanaa na Michezo usiku wa kuamkia leo.

Katika fainali hii timu ya Real Madrid imeibuka bingwa wa  kombe la UEFA wa mwaka huu baada ya kuibamiza Liverpool bao moja katika kipindi cha pili cha mchezo.

Ameongeza kuwa  sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo nguvu shawishi za taifa lolote duniani.

Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuitangaza na kuifungua Tanzania duniani kupitia Filamu ya Royal Tour.

Kabla ya mechi hiyo mamia ya watu waliohudhuria waliopata fursa ya kuangalia Filamu hiyo ya Royal Tour.

Ameongeza kuwa Wizara kwa kushirikiana na wadau  wataratibu tukio  maalum la kuionesha  Filamu ya Royal Tour kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijijini ili wananchi wengi waweze kupata fursa ya kuiangalia.

Aidha, amewataka wadau mbalimbali wa sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea  kushirikiana na Wizara   katika kuleta mapinduzi makubwa  kwenye sekta hizo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Kampuni ya kinywaji cha Heineken nchini ambayo ndiyo aliyedhamini kuonyesha mubashara fainali hizo hapa nchini kupitia DSTv amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa faida wananchi wa Tanzania.

Katika tukio hilo Mhe. Waziri aliambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu na Watendaji wengine wa Wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.