Habari za Punde

DC Moyo Awaomba Wadau na Makampuni Kuwekeza Kwenye Mchezo wa Volleyball.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Hassan Moyo akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kuwekeza kwenye mchezo wa volleyball ili nao uweze kuongeza ajira kwa vijana na wananchi.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

WACHEZAJI wa mpira wa wavu kutoka katika mikoa mitano ya Tanzania Bara wamewaomba wadau,taasisi mbalimbali na makampuni kujitokeza kudhamini mashindano mbalimbali ya mpira wa wavu kwa kuwa umekuwa mmoja ya mchezo ambao umerudisha mvuto kama ilivyokuwa awali.


Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa ufundi wa mashindano ya One Africa volleyball Roben Msigwa alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa yanakuwa siku hadi siku kutokana na mvuto wa mashindano yenyewe.


Alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji vipya vya wachezaji wa mchezo ambao umekuwa adimu kwenye baadhi ya mikoa hivyo kupitia mashindano hayo itakuwa chachu ya kukuza mchezo huu kwenye mikoa ya jirani.


Msigwa alisema kuwa timu ambazo zilishiliki mashindano hayo ya One Africa ni timu nane ambazo ni Mafinga,Mkwawa,Tumain,Notouris,Best Six,Combine na Kampala zikiwa zimetoka katika mikoa mitano ambayo ni mkoa wa Iringa,Mbeya,Ruvuma,Dodoma na Dar es salaam ambazo zilikuwa na wachezaji zaidi ya mia moja.


Alisema kuwa wamekuwa wakichangishana kuhakiksha  wanafanikisha kufanyika kwa mashindano hayo hivyo wanawaomba wadau,taasisi na makampuni mbalimbali kuwekeza au kudhamini mchezo wa mpira wa wavu ambao unamashabiki wengi.

 

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ambaye alikuwa mgeni  katika uzinduzi wa mashindano alisema kuwa kunahaja ya viongozi wa michezo wilaya ya Iringa kuhakikisha wanauzingatia mchezo huo ili uwe unachezwa kwenye viwanja vilivyopo mkoani Iringa.


Moyo alisema kuwa mchezo huo umekuwa unachezwa kwenye mikoa ya uwanda wa pwani na baadhi ya mikoa hivyo lazima kuwekeza nguvu na kuunganisha wadau na makampuni mengine kuwekeza kwenye mchezo huo ambao umekuwa na mashabiki wengi hivi sasa.

 

Aliwataka maafisa elimu waliopo katika wilaya ya Iringa kuweka mikakati ya kufundisha mpira wa wavu ili watoto wanavyokuwa wanakuwa huku wakijua kuwa kunamchezo mwingine ambao unaitwa volleyball ambao unafaida pia kwa afya na ajira.


Moyo aliwataka vijana wa wilaya ya Iringa kutumia michezo kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchukua mikopo inayotolewa na halmashauri ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijana.

 

Nao baadhi ya wachezaji wa mchezo huo waliwaomba wadau kujitokeza kuwekeza kwenye mchezo huo wa mpira wa wavu ambao umekuwa mchezo pendwa kwa jamii ya wanamichezo.

Walisema kuwa mashindano ya One Africa yamekuwa mashindano ambayo yanawakutanisha watu kutoka mikoa mbalimbali na kuibua upya ya kupambanania na kuukuza mchezo huo.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya chuo cha Kampala nchini Tanzania
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mafinga mkoani Iringa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.