Mwanachama wa CCM Omar Ramadhan Issa akimuuliza swali Mratibu wa Sensa na Makakazi ya watu kuhusu mwananchi mwenye zaidi ya nyumba tatu vipi mtuhuyo ataisabiwa katika sensa hiyo.
Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
Na Khadija Khamis- Maelezo 16/06/2022.
Jamii imetakiwa kushiriki zoezi la sensa ya watu na makaazi ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti mwaka huu.
Hayo ameyasema Mratibu wa Sensa ya Watu na Makaazi Tanzania Zanzibar Abdulmajid Jecha Ramadhani wakati akitoa mafunzo kwa wanamaskani ya Kachorora kuhusiana na zoezi la sensa ya watu na makaazi katika mukumbi wa maskan hiyo.
Amesema zoezi la sensa ni la kitaifa Kila mtu anawajibu wa kuhesabiwa ambae amelala ndani ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Aidha alifahamisha kuwa watu wote watakaohesabiwa ambao watalala usiku wa kuamkia siku ya sensa katika Kaya zao na iwapo mkuu wa Kaya atakuwa na kaya zaidi ya moja atahesabiwa sehemu ambayo aliyolala kwa siku ile.
Amesema umuhimu wa sensa ni kujua idadi ya watu na mahitaji yao na kutathmini upungufu wa huduma za kijamii ikiwemo elimu,Afya ,umeme, maji safi na salama hali ya ajira miundombinu na kadhalika kwa lengo la kuleta maendeleo ya wananchi .
Alifahamisha kuwa kila mtu anahitaji kushiriki katika sensa ya watu na makaazi kwani kutokushiriki kutasababisha kuwa njima fursa za kupata huduma watu wengine .
Nae Katibu wa maskani ya kachorora Mtumwa Othman amesema lengo la kuwapatia mafunzo ya sensa kwa wanachama wa chama cha mapinduzi ni kuiunga mkono serikali katika zoezi hilo la kitaifa .
Alieleza mafunzo hayo yatasaidia kuwapatia elimu wanachama hao ili kuwa mabalozi kwa wengine lengo ni kufanikisha malengo ya zoezi hilo.
Nao wanachama wa maskani ya kachorora wamesema wameridhika na mafunzo ya sense ya watu na makaazi waliyoyapatiwa na watashiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kuwataka watu wote washiriki bila ya kujali dini kabila na jinsia na chama kwani kila mtu anahitaji kuhesabiwa.
No comments:
Post a Comment