Habari za Punde

WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA TIMU YA WANAWAKE YA KRIKETI KWA KUONGOZA RWANDA

Na John Mapepele.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Tanzania ya  Wanawake ya Kriketi kwa kufanya vizuri na kuongoza kwenye mashindano ya Kwibuka Cup yanayoendelea nchini hivi sasa nchini Rwanda.

Mhe. Mchengerwa ametoa pongezi hizo leo Juni 15, 2022 alipoongea na simu timu hiyo kupitia kwa Nahodha wa timu hiyo .

Amesema anaipongeza timu hiyo  baada ya kuzishinda timu zote walizokutana nazo kwenye mashindano hayo na kuwa kinalani mwa mashindano hayo.

Amezitaja timu hizo kuwa ni Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana na  Ujerumani  bado timu ya Nigeria na Brazil ambapo wakishinda mechi mojawapo wanaingia fainali za mashindano hayo.

Aidha, amemshukuru Balozi wa Tanzania nchini Rwanda Mhe.  Meja Jenerali Richard Makanzo  kwa kuwa karibu na timu hiyo katika kipindi chote huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuisaidia timu hiyo ili ifike mbali zaidi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.