Habari za Punde

Tamasha la Nchi za Jahazi (ZIFF) Latimiza Miaka 25 Tangu Kuazishwa Kwake Zanzibar.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita akizungumza na Uongozi wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF)  walipofika Ofisini kwake Migomani Unguja kwa mazungumzo na kutowa taarifa ya matayarisho ya Tamasha hilo  linalotarajiwa kufanyika mwezi huu 18-26 katika viwanja vya Ngome Kongwe na kutimia miaka 25 Tangu kuazishwa kwake Zanzibar.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar Mhe. Tabia Maulid Mwita akizungumza na Uongozi wa Tamasha la Nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF) , walipofika Ofisini kwake Migomani Unguja kwa mazungumzo na kutowa taarifa ya matayarisho ya Tamasha hilo  linalotarajiwa kufanyika mwezi huu 18-26 katika viwanja vya Ngome Kongwe na kutimia miaka 25 Tangu kuazishwa kwake Zanzibar
Mkurugenzi Mtendaji Tamasha la nchi za Jahazi Zanzibar  (ZIFF)Profesa Martin Mhando akizungumza wakati wa mkutano wao na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita, uliofanyika katika Ofisi ya Waziri Migombani Unguja, na kusema mwaka huu kutakuwa na filamu mia moja na tano kwani wamepokea nyingi katika usajili.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita akimsikiliza  Mkurugenzi Mtendaji Tamasha la nchi za Jahazi Zanzibar (ZIFF) Profesa Martin Mhando akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Ofisi ya Waziri Migombani Unguja, na kusema mwaka huu kutakuwa na filamu mia moja na tano kwani wamepokea nyingi katika usajili.

WAZIRI  wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita amesema Serikali itaendelea na mkakati wa kutafuta wadhamini sekta binafsi ili kukuza tamasha la  majahazi nchini.

Ameyaeleza hayo wakati alipokutana na uongozi wa ZIFF katika ukumbi wa Wizara ya Habari Migomabani, alisema mkakati huo utasaidia kuleta mabadiliko mbali mbali ya tamasha ili kusudi kuendeleza utamaduni.

Alisema ZIFF imekuwa na mwamko kwa wananchi katika shughuli zao za ujasiriamali, filamu, tamaduni mbali mbali  wanazozifanya hivyo ni vyema kufanyika na kulithamini kwani linasaidia kukuza uchumi wa nchi.

Mkurugenzi Mtendaji Tamasha la nchi za Majahazi Profesa Martin Mhando alisema mwaka huu kutakuwa na filamu mia moja na tano kwani wamepokea nyingi katika usajili.

Alisema watu wengi wamekuwa wakitaka filamu zao kuonekana katika tamasha  kwani  linafatiliwa  filamu zake kimataifa kutokana na hadhi ya Zanzibar.

Tamasha la nchi za majahazi linatarajiwa kuanza Juni 18-26 huko Ngome Kongwe ambapo linatimiza miaka 25 tokea kuazishwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.