Habari za Punde

Tanga Uwasa Yatumia Zaidi ya Milioni 150 Kuagiza Mita Malipo Kabla Nchini Ufaransa.

 

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani
kuhusiana na tuzo walizopata katika maonyesho ya 9 ya Biashara yaliyofanyika Jijini hapa

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban katikati akiwa amebeba Kombe la Ushindi na tuzo ikiwa chini akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo kwenye Banda lao mara baada ya kukabidhiwa
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban katikati akiwa amebeba Kombe la Ushindi na tuzo ikiwa chini akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo kwenye Banda lao mara baada ya kukabidhiwa

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban amesema mamlaka hiyo imetumia zaidi ya Shs Milioni 150 kwa ajili ya kuagiza mita za malipo ya kabla (pre-paid)toka Nchini Ufaransa.
Mhandisi Shabani aliyasema hayo  wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo walizopata katika maonyesho ya 9 ya Biashara yaliyofanyika Jijini hapa.

Mhandisi Shabani alisema kumekuwepo na malalamiko kwa wateja yanayohusu madai ya kuongezewa gharama za malipo(bili) ambapo mita hizo ndio zitakuwa muarobaini wa malalamiko hayo.

Aidha alisema Mamlaka hiyo imefanya tafiti za kutosha na kubaini kwamba wananchi wengi hawajatambua tatizo la ongezeko la bili ya maji hivyo kuanza kutafuta mbinu mbadala ya kumaliza tatizo hilo.

Alisema lengo ni kukidhi hitaji la Serikali la kutaka wananchi waweze kupata huduma ya maji katika maeneo yote kwa Mijini na Vijijini.

“Tumeanza kufanya tathmini kama tulivyoagizwa na Wizara kuhusiana na mita hizi za malipo ya kabla(pre-paid) na tathmini yetu iko vizuri na matarajio yetu tutafanikiwa”Alisema Mhandisi Shaaban.

Alisema matarajio kuanza na mita 500 ambapo Mamlaka hiyo imepanga kuzifunga kwa baadhi ya wateja kama sehemu ya majaribio na mafanikio yake ndio yatakayopelekea kufungwa kwa mita hizo Mkoa Mzima.

“tumeshaanza majaribio ya mita hizo na zinaonekana kuwa na tija lengo letu sasa ni kuhakikisha tunazisambaza Mkoani kote ”Alisema Mhandisi Shaaban.

Mhandisi Shabani alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi Mkoani Tanga kupokea huduma hiyo na watakuwa na uwezo wa kununua maji kutokana na uwezo wa mteja kama inavyofanyika katika huduma nyingine za kijamii.

Hata hivyo alisema Mamlaka hiyo imepokea tuzo ya watoa huduma bora dhidi ya Mamlaka za Serikali zilizokuwepo kwenye maonyesho hayo kwa kupatiwa cheti na ngao na ile ya ushindi wa Jumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.