Habari za Punde

TMDA: Matumizi ya Tumbaku Yanaweza Kusababisha Matatizo Kwenye Via vya Uzazi.

Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja wa TMDA Roberta Feruzi akitoa elimu kwa wananchi waliojitokeza kwenye banda lao kwenye eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakoendelea Maonyesho ya Biashara na Utalii Jijini Tanga

Na.Oscar Assenga -TANGA

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba nchini (TMDA) imesema kwamba matumizi ya tumbaku yanaweza kusababisha matatizo kwenye via vya uzazi,athari ya kansa ya utumbo mpana na kupoteza nguvu kazi ya Taifa na hivyo kusababisha Serikali kutumia fedha nyingi katika kutibu magonjwa hayo

Hivyo wito ulitolewa kwa wananchi kuacha kutumia tumbaku,uvutaji wa sigara
kutokana na kwamba ni hatari kwa afya zao na athari zake ni kubwa kwa jamii hivyo waache matumizi yake

Hayo yalisemwa na Afisa Mwandamizi wa Elimu kwa Umma na Huduma kwa wateja Roberta Feruzi wakati akizungumza n waandishi wa habari katika eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya 9 ya viwanda,biashara na talii Jijini Tanga.

Alisema wameshiriki maonyesho hayo ili kuweza kutoa elimu kwa wananchi wao kama mamlaka ya dawa wamepewa dhamana ya kusimamia na kudhibiti bidhaa za tumbaku huku wakitoa wito kwa wananchi kuacha kutumia

Aidha alisema wao wanalinda kwa kuelekeza kwamba bidhaa za tumbuka watu waache kutumia bidhaa hizo kwani zimekuwa na athari kubwa sana kwa wananchi  kidogo kidogo ikiwemo kansa lakini kubwa zaidi ni nguvu kazi ya uzalishaji mali kwa maendeleo ya Taifa inapungua .

 “Lakini kubwa ni kundi cha chini ya miaka 18 limekuwa likijiingiza kwenye uvutaji wanatoa wito waache mara moja kwani mandhara yake ni makubwa kwa jamii “Alisema

Hata hivyo alisema wameshiriki kwenye maonyesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi waifahamu taasisi lakini kazi yao kulinda ubora wa jamii wanailinda kwa kusimamia ubora,usalama na ufanisi wa bidha za dawa,vifaa tiba na vitenganishi.

“Lakini pia kusimamia uzibiti wa bidhaa zinazotokana na tumbaku,TMDA kuhakikisha jamii na wanatoa elimu juu ya matumizi sahihi ya dawa wengi wamekuwa wakikiuka matumizi ya dawa ipasavyo kutokana na kutokupata elimu na kupelekea matatizo kwenye mwili na usugu vimilea”Alisema

Hata hivyo alisema pia wanatoa elimu juu ya utoaji wa tahadhari ya mauzi yanatoweza kutokana na maudhi ya bidhaa za dawa,vifaa tiba na vitengenishi waweze kutoa taarifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.