Habari za Punde

Ubingwa wa Klabu ya Yanga African Umeleta Mshakamano - Mhe. Mchengerwa.

Kikosi cha Klabu ya Yanga African Wakishangilia Ubingwa wao baada ya kukabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania ya NBC Primier League kwa msimu wa mwaka 2021/2022.

Wapenzi na  Mashabiki wa Klabu ya Yanga African wakishangilia Klabu yao wakati wa mapokezi
Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Tanzania Mhe.Mohamed Mchengerwa  akizungumza na kuipongeza Klabu ya Yanga African kwa kuchukubi Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa msinu wa mwaka 2021/2022.

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa ameipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa kombe la katika ligi Kuu ya NBC katika msimu huu.

Mhe. Mchengerwa  ameipongeza Klabu ya Yanga kwa kuchukua Ubingwa huo huku akipongeza mshikamano na furaha za mashabiki, ambazo wamezionyesha  wakati wa kukabidhiwa kombe hilo na mapokezi yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

" Kwa aina ya shangwe za ubingwa zilizofanyika jana na leo ni sawa na zile za mataifa yaliyoendelea ya Ulaya. Hakika mpira wa miguu ni mchezo mkubwa na pendwa duniani ambao huwaunganisha watu pamoja na kuleta amani, mshikamano, furaha na umoja baina ya wananchi"

Ameongeza kuwa watanzania zaidi ya 90% ni wapenzi wa mchezo wa soka na amesisitiza kuwa serikali itaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha inaboresha miundombinu ya michezo na kuleta usawa katika michezo hasa mpira wa miguu ili  kila mtanzania aweze kupata furaha.
 
"Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa watanzania wanaendelea kupata furaha na faraja katika  michezo" amesisitiza Mhe . Mchengerwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.