KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu (kulia), akimsikilzia kwa makini Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, Bw. James Mlowe alipotembelea banda hilo la Ushirikiano. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Bi. Aisha Sango.
NA
KHALFAN SAID, SABASABA
KATIBU
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal
Katundu ametembelea banda la USHIRIKIANO linalotumiwa kwa pamoja na Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF) katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ili kujionea
jinsi watumishi wa Mifuko hiyo iliyo chini ya Ofisi yake wanavyotoa huduma kwa
wanachama wao na wananchi kwa ujumla.
Alipowasili
kwenye banda hilo alipokelewa na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF Bw. James
Mlowe na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF Bi. Aisha Sango.
Profesa
Katundu alitembezwa katika idara mbalimbali za mifuko hiyo ikiwa ni pamoja na
kuzungumza na watoa huduma (watumishi), wananchama na wananchi waliotembelea
banda hilo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
yanayoendelea kwenye viwanja hivyo vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba.
Akiwa
katika banda la PSSSF Profesa Katundu pia alijionea Tangawizi iliyochakwa inayozalishwa
na kiwanda kinachomilikiwa kwa ubiya
baina ya PSSSF na wanaushirika wa Mamba Miamba, jimbo la Same mkoani
Kilimanjaro ambapo alifurahia ubora wake.
Maonesho
hayo ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yenye kauli mbiu isemayo “Tanzania
Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji,” yalianza Juni 28 na yanatarajiwa
kufikia kilele Julai 13.
No comments:
Post a Comment