Habari za Punde

Waziri Mhe.Simbachawene Apongeza Utekelezaji wa Oporesheni Anwani za Maakazi Kibwakwe.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene akikagua utekelezaji wa Operesheni anwani Makazi katika Kijiji cha Mpwanila kata ya Luhundwa katika jimbo la Kibakwe Halmashauri ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene akikagua utekelezaji wa Operesheni anwani Makazi katika Kijiji cha Ikuyu kata ya Luhundwa katika jimbo la kibakwe halmashauri ya Mpwapwa.

Na mwandishi wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Geroge Simbachawene amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kwa kutekeleza vizuri zoezi la anwani za makazi.

“Uwekaji wa anwani za makazi unaenda sambamba na zoezi la sensa ili kujua katika ramani mahali mitaa, barabara zilipo. Mmefanya jambo zuri ambalo watu wengine wanapaswa kuja kujifunza alisema waziri”

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu (Mb) Mhe George Simbachawene katika ziara aliyoifanya Kata ya Pwaga na  na Luhundwa alipotembelea na kufanya Mikutano.

“Haya ni maelekezo ya Mhe. Rais  Samia Suluhu Hassan ambaye aliagiza operesheni ya postikodi ili watanzania  wajulikane wanakaa wapi; jambo la kuweka mitaa, lakini pia barabara na namba kwenye nyumba katika Halmashauri wilaya ya Mpwapwa na jimbo la Kibakwe limefanyika kwa mazingira makubwa”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.