Habari za Punde

Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi Akabidhiwa Vifaa Kwa Ajili ya Wanawake Wajasiriamali wa Utengemezaji wa Sabuni za Mwani na Kampuni ya CRJE.

MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa mashine ya kuchanganya unga wa mwani kwa ajili ya utengenezaji wa sabuni na Meneja wa Kampuni ya CRJE Bw.Shi Yan, hafla hiyo ya kukabidhi vifaa hivyo uliofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo migombani Unguja.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambe ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akiangalia kifaa kwa ajili ya utengeneza sabuni, baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Kampuni ya CRJE Tawi la Zanzibar Bw.Shi Yan (kulia) kwa ajili ya Vikundi vya Wajasiriamali wa Mwani Zanzibar.
MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa glovzi kwa ajili ya matumizi ya utengenezaji wa sabuni ya mwani na Meneja wa Kampuni ya CRJE Tawi la Zanzibar Bw. Shi.Yan, hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Kampuni ya CRJE kwa ajili ya Vikundi vya Wanawake wa Kilimo cha Mwani Zanzibar, iliyofanyika katika Ofisi za Taasisi hiyo Migombani Unguja.

MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mama Mariam Mwinyi akizungumza na ujumbe wa Kampuni ya CRJE, walipofika katika Ofisi za Taasisi hiyo migombani Unguja kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vifaa vya utengenezaji wa Sabuni ya Mwani kwa ajili ya Vikundi vya Wajasiriamali wa bidhaa za mwazi Zanzibar

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi  ametoa pongezi kwa Kampuni ya ujenzi ya CRJE ya nchini China kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwawezesha wanawake wakiwemo wakulima wa mwani.

Mama Mariam Mwinyi aliyasema hayo leo huko ofisini kwake Ikulu ndogo Migombani, Zanzibar wakati alipokutana na uongozi wa Kampuni ya ujenzi ya CRJE ya nchini China.

Katika mazungumzo yake, Mama Mariam Mwinyi alitoa pongezi kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwasaidia katika kunyanyua hali za maisha za wanawake na Wazanzibari kwa ujumla.

Alisema kwamba hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwasadiia akina mama wanaolima mwani kwa kuwaweka salama kutokana na kutoa misaada kadhaa ikiwemo vifaa vya kulimia mwani, viatu, glavu, dawa za kuchanganya sabuni, mabeseni kwa ajili ya matumizi ya kutengezea sabuni pamoja na vifaa vya sabuni.

Sambamba na hayo , Mama Mariam Mwinyi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya ‘Zanzibar Maisha Bora Foundation’ (ZMBF), alieleza haja kwa uongozi wa Kampuni hiyo ya kusaidia zaidi kwa lengo la kuwaongezea uwezo wanawake katika kilimo cha mwani.

Aliongeza kuwa akina mama wanaolima mwani wanahitaji vitu katika kufanikishwa katika wanavyovifanya na hivi sasa kinachozingatiwa zaidi hivi sasa ni kuongeza ubora katika bidhaa zao.

Nae Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya CRJE ya nchini China, Yussuf Fabian Saimon, alitoa shukurani kwa Mama Mariam Mwinyi kwa ukaribisho wake na kusema kwamba CRJE hapa Zanzibar imeanza tokea mwaka 2003 huku akieleza majengo kadhaa yaliyojengwa hapa Zanzibar na Kampuni hiyo.

Katika maelezo yake Meneja huyo alisema kwamba kwa vile Kampuni yake inafanya kazi na Serikali imeona ni vyema kile wanachokipata watoe msaada wao kwa Serikali na wananchi kwa ujumla wakiwemo wakulima wa mwani.

Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.