Habari za Punde

PBZ Yakabidhi Msindi wa Bodaboda Kwa Wakala wa PBZ.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Dkt. Muhsin Salim Masoud akimtangaza mshindi wa  Bodoboda PBZ Wakala, wakati wa mchezo wa Ngao ya Hisani ya Michuano ya Yamleyamle ZBC Uwanja wa Amaan Unguja, mshindi wa shindano hilo na Wakala wa PBZ Ndg.Kassim Salum na kukabidhiwa Bodaboda yake.(kushoto kwake) Meneja wa Masoko wa PBZ Ndg. Seif, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dkt.Estella Ngoma Hassan na Afiusa Masoko wa PBZ Ndg. Mohammed.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PBZ Dkt.Estella Ngoma Hassan akimkabidhi mshindi wa Bodaboda PBZ Wakala Ndg. Kassim Seleiman kwa kuibuka mshindi kwa kutowa hudima ya kibenki kupitia Wakala (katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Dkt.Muhsin Salim Masoud.hafla hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Amaan Unguja wakati wa mchezo wa Ngao ya Hisani ya Ufunguzi wa Michuano ya Yamleyamle Cup.
Mshindi wa Bodaboda PBZ Wakala Ndg. Kassim Suleiman akishangilia na Wafanyakazi wa PBZ baada ya kukabidhiwa Pikipiki (Bodaboda) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PBZ Dkt.Estella Ngoma Hassan.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.