Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Ameweka Jiwe la Msingi Jengo la Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba na Kukabidhi Vifaa kwa Wakulima wa Mwani.

MUONEKANO wa Jengo Jipya la Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba likiendelea na Ujenzi wake na kuwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.,Hussein Ali Mwinyi, wakati wa ziara yake Pemba kutembelea Miradi ya Maendeleo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya Kitaalam ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba kutoka kwa Mhandisi wa Wizara ya Afya Ndg. Said Ali Bakari,wakati akitembelea jengo hilo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wake,na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Salama Mbarouk na Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh Khamis
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa Pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba akiwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh Khamis na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya Kitaalam ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba kutoka kwa Mhandisi wa Wizara ya Afya Ndg. Said Ali Bakari,wakati akitembelea jengo hilo baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wake,na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Salama Mbarouk na Naibu Waziri Wizara ya Afya Zanzibar Mhe. Hassan Hafidh Khamis.

RAIS wa Zanzibar wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mjasimriamali wa bidhaa mbalimbali wakati wakitembelea maonesho ya Wajasiriamali wa Mkoa wa Kaskazini Pemba yaliofanyika katika viwanja vya mpira Micheweni Pemba.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Vifaa vya kulimia Mwaniu Mjasiriamali Bi. Zuma Omar Faki,  hafla hiyo ya kukabidhi Vifaa vya Kilimo cha Mwani iliyofanyika katika viwanja vya mpira Micheweni Pemba na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mratibu Mradi wa URT.Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania Ndg.Joseph Kihaula.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.