Habari za Punde

SMZ na Serikali ya Oman Yakagua Eneo Linalotarajiwa Kujengwa Hospitali ya Mkoa Mahonda Unguja.

Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazurui akimuonyesha Katibu Mkuu Wizira ya Mambo ya Nje wa Oman Mhe.Mohammed Naseer Al-Wahaibi na ujumbe wake baadhi ya Mipaka katika eneo ambalo linatarajiwa  kujenga Hospitali ya Mkoa ,huko Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja,  kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Oman.

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar.                                                                             

Serikali ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Oman inatarajia kujenga Hospitali ya Mkoa Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja  ili kuondosha msongamano wa wagonjwa katika haspitali kuu ya Mnazimmoja.

Akizungumza mara ya baada ya kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa Hospitali hiyo, Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazurui amesema lengo la kujengwa Hospitali hiyo ni kupanua zaidi huduma za Afya  kwa wananchi ili waweze kupata matibabu bora nchini.

Amesema uwepo wa hospitali hiyo ni kutimiza adhma ya Serikali ya awamu ya nane katika kuhakikisha kila mkoa kunakua na  hospitali ya mkoa  ambayo itasaidia wananchi waliowengi kupata matibabu hasa vipimo vya C-SCAN,MRI, ULTRASOUND pamoja na X-RAY ambavyo havipatikani katika vituo vya afya.

Aidha Waziri Mazurui amefahamisha kuwa katika hospitali hiyo kutakua na vifaa vyote vinavyohitajika, ikiwemo dawa za kutosha  na madaktari wenye sifa ambao watashughulikia wagonjwa na kuhakikisha kila mzanzibar anapata matibabu bila ya kwenda nje ya nchi.

Nae Mkuu wa Mkoa huo Ayoub Moh’d Mahamoud amesema kuwa ujio wa Serikali ya Oman kutaka kujenga Hospital hiyo   ni utekelezaji wa agizo la   Rais wa Zanzibar alilolitoa hivi karibuni  katika ziara yake Mkoani humo.

Amesema kuwa eneo hilo linalotarajiwa kujengwa hospitali hiyo ni la Serikali wameamua kufanya hivyo kutokana na kupanuka kwa harakati za wananchi ambapo wanategemea kupata fursa mbalimbali kwa wananchi wa mkoa huo.

Kwa upande wake  Balozi mdogo wa Oman nchini Tanzania Said Salim Al sinawi amesema wameamua kujenga hospitali hiyo ili kuondosha usumbufu kwa wanannchi wa mkoa huo katika kufuata huduma hiyo masafa marefu.

Aidha Balozi huyo amefahamisha kuwa ujenzi wa Hospital hiyo unatarajiwa kuanza kabla ya kumalizika kwa mwaka huu ambapo baada ya kukamilika kwake hospitali hiyo itahudumia wagonjwa wengi zaidi wa Mkoa huo. 

Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazurui akimuonyesha Katibu Mkuu Wizira ya Mambo ya Nje wa Oman Mhe.Mohammed Naseer Al-Wahaibi na ujumbe wake baadhi ya Mipaka katika eneo ambalo linatarajiwa  kujenga Hospitali ya Mkoa ,huko Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja,  kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Oman.
Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazurui akimuonyesha Katibu Mkuu Wizira ya Mambo ya Nje wa Oman Mhe.Mohammed Naseer Al-Wahaibi na ujumbe wake baadhi ya Mipaka katika eneo ambalo linatarajiwa  kujenga Hospitali ya Mkoa ,huko Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja,  kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Oman.
Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazurui akizungumza na Ujumbe kutoka Serikali ya Oman mara baada ya kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa Hospitali ya Mkoa ,huko Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja
Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Nassor Ahmed Mazurui akimkabidhi zawadi maalum  Katibu Mkuu Wizira ya   Mambo ya Nje wa Oman Mhe.Mohammed Naseer Al-Wahaibi mara baada ya kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa Hospitali ya Mkoa ,huko Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja  Ayoub Moh’d Mahamoud akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa Huko Mahonda  Wilaya ya Kaskazini “B’ Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakati wa ukaguzi wa Eneo linalotarajiwa kujengwa Hospitali hiyo uliofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishirikiana na Serikali ya Oman.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.