Habari za Punde

Dkt. Nchemba Aomboleza Kifo cha Diwani Kilichotokea kwa Ajali ya Gari

Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akieleza kuhuzunishwa na kifo cha aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Kinampanda Wilayani Iramba Singida, Bi. Winzuka Mkumbo, kilichotokea kwa ajali ya gari na kuzikwa kijijini kwake  Simbalugwala Wilayani hapo.

Na. Peter Haule, WFM, Singida

Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameahidi kuchangia gharama za masomo kwa watoto wa aliyekuwa Diwani wa viti maalum tarafa ya Kinampanda Iramba, Bi. Winjuka Mkumbo, aliyefariki kwa ajali ya gari iliyotokea Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Dkt. Nchemba alitoa ahadi hiyo wakati wa mazishi ya Diwani huyo yaliyofanyika Kijiji cha Simbalugwala Kata ya Mukulu Wilayani Iramba Mkoani Singida.

Alisema kuwa kifo cha aliyekuwa Diwani, Bi. Winjuka kimemsikitisha sana kwa kuwa licha ya utendaji kazi wake uliotukuka, alikuwa rafiki wa karibu wa familia yake.

“Naahidi kugharamia ada za watoto wa marehemu ambao wapo katika ngazi mbalimbali za elimu ili waweze kutimiza ndoto zao ”, alisema Dkt. Nchemba

Alisema kuwa marehemu alikuwa mchapakazi aliyeyapenda maendeleo ya wananchi na nchi yake na wakati wote alihubiri umoja, upendo na mshikamano.

Alisema kuwa watu wengi waliojitokeza kuuga mwili wa marehemu ni ishara ya kuwa aliishi vizuri na watu na hivyo ni vema na wengine wajifunze yale mema ambayo marehemu aliyafanya enzi za uhai wake.

Kwa upande wao viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, wameitaka Serikali kuendelea kudhibiti ajari za barabarani ili kupunguza kupoteza nguvu kazi muhimu ambayo ingeongeza kasi ya maendeleo kwa kulitumikia taifa katika nyanja mbalimbali.

Aidha waliwashukuru waombolezaji kwa mshikamano wao katika kuhakikisha wanamsitiri kwa heshima marehemu katika nyumba yake ya milele.

Kwa upande mwingine viongozi hao waliwataka waombolezaji kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ambayo inatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 23 mwaka huu ili kuweza kuisaidia Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa ajili ya manufaa ya wananchi hao.

Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwa na madiwani wa Wilaya ya Iramba, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Kinampanda Wilayani Iramba Singida, Bi. Winzuka Mkumbo, aliyefariki kwa ajali ya gari.
Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Kinampanda Wilayani Iramba Singida, Bi. Winzuka Mkumbo, aliyefariki kwa ajali ya gari.
Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Kinampanda Wilayani Iramba Singida, Bi. Winzuka Mkumbo, aliyefariki kwa ajali ya gari na kuzikwa kijijini kwake  Simbalugwala Wilayani hapo.
Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Kinampanda Wilayani Iramba Singida, Bi. Winzuka Mkumbo, aliyefariki kwa ajali ya gari.

Waziri wa Fedha na Mipango na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akimfariji mfiwa wakati wa mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Kinampanda Wilayani Iramba Singida, Bi. Winzuka Mkumbo, aliyefariki kwa ajali ya gari na kuzikwa kijijini kwake  Simbalugwala Wilayani hapo.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Singida)


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.