Habari za Punde

Makabidhiano ya Ujenzi wa Barabara na Miundombinu Eneo la Uwekezaji Micheweni Pemba Baina ya ZIPA na UUB.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Ndg. Sharif Ali Sharif (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar Mhandisi Mbaruk Juma Mbaruk  mkataba wa Ujenzi wa Makabidhiano ya Maeneo Huru ya Uchumi Micheweni baina ya ZIPA na Wakala wa Barabara (UUB) kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya kilomita 13.6 na miundombinu mengine. kazi hiyo itaanza rasmi na itakabidhiwa serikalini baada ya miezi mitatu

Mamlaka ya Kukuza uwekezaji Zanzibar ZIPA na Wakala wa Ujenzi wa Barabara UUB leo wametiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara katika maeneo ya uwekezaji Micheweni Pemba.

Mkurugenzi Mtendaji  Nd. Sharif Ali Sharif akiweka saini kwa niaba ya ZIPA amesema hatua hiyo inafikiwa baada ya makubaliano ya pande mbili na ujenzi unatarajiwa kuanza mapema iwezekanavyo, na utakuwa wa kiwango cha hali ya juu ya kushajihisha uwekezaji Zanzibar.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Engineer Mbaruk Juma Mbaruk ameishukuru ZIPA kwa kuwaamini kuwapa ukandarasi huo....na wanaahidi kwenda kama makubaliano yalivyojieleza na kazi itakabidhiwa ndani ya miezi mitatu kuanzia sas.

Ujenzi wa miundo mbinu ya barabara Micheweni utaongeza fursa za uwekezaji kisiwani Pemba ambapo eneo hilo linatarajiwa kuekezwa kwa ujenzi wa mji mpya ikowemo .. maskuli, veranda, viwanja vya michezo, hosptali na makaazi.

Aidha hatua hiyo inaungana mkono na kauli mbiu ya mhe. Rais ya kuifungua Pemba kiuwekezaji na Utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Ndg. Sharif Ali Sharif akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar (UUB) Mhandisi Mbaruk Juma Mbaruk wakitembelea eneo la Uwekezaji Micheweni Pemba baada ya kukabidhiwa kwa Ujenzi wa Barabara na Miundombinu mengi katiuka eneo hilo la Uwekezaji katika Mkoa wa Kaskazini Pemba. 
Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Ndg. Sharif Ali Sharif (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Zanzibar Mhandisi Mbaruk Juma Mbaruk na Maofisa wa ZIPA na wa UUB, baada ya kukabidhiana eneo hilo kwa ajili ya Ujenzi wa Barabara na Miundombinu mengi kwa ajili ya Uwekezaji katika eneo hilo la Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.   
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.