Habari za Punde

Waziri Mhe Lela Mohammed Mussa Amewataka Watendaji wa Wizara ya Elimu Pemba Kusimamia Miradi ya Ujenzi ya Wizara Kuhakikisha Inajengwa kwa Kiwango.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na kuwata kuendelea kusimamia miradi ya Ujenzi ya Wizara ya Elimu Ili kuhakikisha kwamba inajengwa kwa kiwango kinachoridhisha.

Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa.(hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na Watendaji hao.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Lela Mohammed Mussa amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu kuendelea kusimamia miradi ya Ujenzi ya Wizara ya Elimu Ili kuhakikisha kwamba inajengwa kwa kiwango kinachoridhisha.

Mh. Lela ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Wafanya kazi wa Idara ya Mipango Sera na Utafiti na Kitengo cha Manunuzi katika Ukumbi wa Afisa Mdhamini Chake Chake Pemba.

Amesema licha ya Kuwepo Mshauri Elekezi bado watendaji wa Idara husika wanawajibu wa kuhakikisha kwamba Miradi ya Ujenzi inatekelezwa kwa ubora wa hali ya juu ili iweze kuleta manufaa yaliyokusudiwa.

Amewataka kutokuona muhali kwa miradi ambayo watabaini udhaifu katika utekelezaji wake na badala yake kuchukua hatua zinazofaa ili kuinusuru miradi hiyo.

Akizungumzia Swala la Vituo vya Maandalizi TuTu Mh. Waziri amewataka watenaji hao kuchukua hatua za dharura katika kuunga mkono Nguvu za Wananchi wa kijiji cha Kanambe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo wanafunzi bado wanasoma chini ya Muembe.

Kwaupande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bw. Ali Khamis Juma amewataka Watendaji hao kuikagua Miradi na na kujiridhisha kabla ya kuipokea kutoka kwa Wakandarasi.

Amewatanabahisha kwamba kupokea mradi wenye mapungufu kunaashiria usimamizi duni wakati wa utekelezaji wa Miradi hiyo hivyo amewataka watendaji hao kutopokea iwapo watabaini mapungufu katika miradi hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.