Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe Hassan Khamis Hafidh na Mwakilishi Mkaazi wa WHO Tanzania pamoja na uongozi wa wizara hiyo wakikabidhiana Vifaa 56 kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa wa Hospitali za Unguja na Pemba yaliyofanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar. Picha N Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Hafidh akiwa katika picha ya pamoja ya pamoja na uongozi kutoka WHO na wizara ya Afya Zanzibar.
Picha N Miza Othman-Maelezo Zanzibar.
Na Bahati Habibu Maelezo 2/9/2022
Naibu Waziri wa Afya Hassan Khamis Hafidh amesema Shirika la Afya Duniani (WHO) limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta ya afya inaimarika nchini na kutoa huduma kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada wa mashine za kupumulia huko ofisini kwake Mnazimmoja amesema msaada huo wenye thamani ya zaidi milioni 77 ambao utasaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi ya kushinda kupumua wanaofika kupata huduma katika vituo na Hospitali mbali mbali.
Amesema tatizo la kupumua limekuwa likiwasumbuwa wananchi wengi hasa wagonjwa pumu na shindikizo la damu hivyo mashine zitasaidia kuuokoa maisha ya jamii inayosumbuka tatizo hilo .
Aidha ameliomba Shirika hilo kuisaidia Zanzibar kupunguza vifo vya mama na mtoto na maradhi ya presha, sukari na saratani ambayo yamekuwa kuongezeka kila siku.
Nae Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani nchini Tanzania Dr Zabulon Yoti amesema shirika lipo tayari kushikrikiana na Serikali ili kuhakikisha kwamba inapunguza na kuondosha vifo vinavyosababishwa na maradhi yasiyoambukiza ambaoyo yamekithiri nchini.
Aidha amesema Shirika hilo litaendelea kutoa msaada wa dawa na vifaa tiba kwa Serikali kwa lengo la kuimarisha sekta ya afya nchini.
No comments:
Post a Comment