Habari za Punde

Mhe Lela alishukuru Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA) kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mohammed Mussa wa pili (kulia), akimkabidhi zawadi Mshindi wa kwanza wa Mashindano ya kuandaa Video za kutangaza Utalii na Utamaduni wa Mzanzibari) Salu Bakar Salum kutoka Taasisi ya Karume. wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa KOICA, Bw.Kyucheol Eo. mashindano hayo  yamefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST), hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Karume  Mbweni Mjini Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mohammed Mussa wa pili (kulia), akimkabidhi zawadi Mshindi wa pili wa Mashindano ya kuandaa Video za kutangaza Utalii na Utamaduni wa Mzanzibari Mwanafunzi wa Taasisi ya Karume Suleiman Saleh Kasim. na wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Karume Dkt. Afua Mohamed.mashindano hayo  yamefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST), hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Karume  Mbweni Mjini Zanzibar.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mohammed Mussa wa pili (kulia), akimkabidhi zawadi Mshindi wa tatu  wa Mashindano ya kuandaa Video za kutangaza Utalii na Utamaduni wa Mzanzibari, Mwanafunzi kutoka Taasisi ya Karume Kassim Moh’d, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume Dkt. Mahmoud Abdulwahab. mashindano hayo  yamefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar (KIST), hafla iliyofanyika katika Taasisi ya Karume  Mbweni Mjini Zanzibar.

NA MARYAM KIDIKO – KIST.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mh.Lela Mohamed Mussa amesema Serikali itaendela kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA) katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya elimu.

Alisema hayo katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya utengenezaji wa video za utalii na utamaduni wa Zanzibar yaliyoandaliwa na Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Korea, yaliyofanyika Mbweni Zanzibar.

Waziri Lela alisema mradi wa mafunzo  ya utengenezaji wa video za utalii uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea ni miongoni mwa ujuzi muhimu kwa vijana, kwani umewawezesha kupata taaluma mpya na pia utawawezesha kujiajiri wenyewe.

Alieleza kuwa, uamuzi uliochukuliwa na  Shirika la Maendeleo la Korea pamoja na Taasisi ya Karume wa kuwafunza vijana ujuzi wa uchukuaji wa video, utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza sekta ya utalii nchini.

Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), Dkt Mahmoud Abdulwahab amesema miongoni mwa  malengo ya kuweka mafunzo hayo ya uchukuaji wa video ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaosoma katika Taasisi ya Karume kuwa na ujuzi wa mambo mbalimbali ambayo yatawasaidia katika maisha yao baada ya kumaliza masomo chuoni hapo.

Aidha alitumia fursa hiyo kulipongeza Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA), kwa ushirikiano mzuri wanaouendeleza katika Taasisis ya Karume katika kufanikisha utoaji wa elimu bora kwa wananchi.

Sambamba na mafunzo hayo wanafunzi watatu miongoni mwa wanafunzi waliopatiwa mafunzo hayo wameweza kuibuka na ushindi wa utengenezaji wa video bora za utalii, ambapo mshindi wa kwanza, alipata zawadi ya Kompyuta yenye thamani ya shilingi 2,300,000, na mshindi wa pili alipata zawadi ya kompyuta yenye thamani ya 1,500,000, na mshindi wa tatu alipata zawadi ya simu aina ya Samsung yenye thamani ya shilingi 1,200,000.

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.