Na Ally Mohammed
Wazazi wametakiwa kuwasomesha vijana ili kupata viongozi bora na wenye kuweza kutoa fatwa kwa kutumia sheria za dini
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ametoa wito huo alipojumuika na Waumini katika Masjid NABAWII Mombasa Mbuyu Mnene wilaya ya magharibi “B” unguja
Ameeleza kuwa ni wajibu wa kila mzazi na mlezi kuhakikisha anawapatia elimu vijana wake ili kuweza kuwa vijana bora wenye kutambua mema na maovu katika nchi
Mhe. Hemed amesema kila mzazi ana jukumu la kuwaanda vijana kuwa viongozi bora wa baadae ambao watasimamia maslahi ya wazanzibari pamoja na kuwa wanazuoni bora.
Alhajj Hemed amewataka waumini na wananchi kwa ujumla kuwasimamia viajna ili kuweza kuondosha chanagamoto zinazoikabili nchi kwa sasa ikiwemo tatizo la madawa ya kulevya na udhalilishaji.
Amesema kuwa ni lazima kila mzazi na mlezi kufanya kila linalowezekana kuwaandaa vijana kwenye kupata elimu bora ambayo itawasaidia hapa duniani na kesho Ahera pamoja na kupata viongozi kwa maslahi ya nchi yetu.
Kwa upande wake Imamu wa Msikiti huo Sheh. SAADAT IMAMU amewataka Waumini na wazanzibari kurudi kwa Allah na kuacha yale yote amabyo yanaweza kuiletea balaa nchi yetu.
Amesema ni wajibu kwa kila muumini kufanya ibada huku akitarajia ujira mkubwa kutoka kwa Allah na kuwataka kufika kwa wakati katika swala zote ikiwemo swala ya ijumaa ili kupata fadhila za allah (S.W)
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Alhajj Hemed amepata fursa ya kumjulia hali Mfanya biashara maarufu nchini MOHAMMED RAZZA nyumbani kwake kibweni wilaya ya magharibi “A” unguja
Amemtaka mfanya biashara huyo kuwa na subra kwa kipindi hichi cha kuumwa kwake na kumuombea duwa kwa mwenyezi mungu kuweza kupona kwa haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kawaida ya ujenzi wa taifa.
No comments:
Post a Comment