Habari za Punde

Zanzibar yaadhimisha siku ya magonjwa ya Moyo Duniani

Wananchi, pamoja na jumuiya ya watoto wanaoishi na magonjwa ya moyo Zanzibar wakiwa katika maandamano maalum katika kuadhimisha siku ya magonjwa ya Moyo Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo September 29 maandamano hayo yalianzia Maisara hadi Muembe Kisonge katika. 
Bendi ya Chuo cha Mafunzo (Magereza) wakiongoza maandamano maalum yaliyoanzia Maisara hadi Muembe Kisonge katika  kuadhimisha siku ya magonjwa ya Moyo Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo September 29. 

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akipokea maandamano maalum yalioongozwa na askari wa Chuo cha Mafunzo katika kuadhimisha siku ya magonjwa ya Moyo Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo September 29, hafla iliyofanyika Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge. 
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akifanya mazoezi ya pamoja na wananchi mbalimbali katika kuadhimisha siku ya magonjwa ya Moyo Duniani huko Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge. 
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akizungumza kuhusiana na magonjwa ya moyo katika maadhimisho ya siku ya magonjwa ya Moyo Duniani yaliyofanyika Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh akisikiliza majibu ya vipimo alivyofanyiwa wakati wa maadhimisho ya siku ya magonjwa ya Moyo Duniani huko Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge. 

Afisa Mahusiano Jumuiya ya Watoto wenye Ugonjwa wa Moyo (OCHZ) Arafa Kombo Suwed akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na changamoto zinazowakabili katika Jumuiya yao wakati wa maadhimsho ya siku ya Magonjwa ya Moyo Duniani yaliyofanyika Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge.

 PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR


Na Rahma Khamis Maelezo                                   29/9/2022

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Hassan Khamis Hafidh ameitaka jamii kuacha kula vyakula vya uwanga kwa wingi na kufanya mazoezi li kujikinga na maradhi yasiyoambukiza ikiwemo maradhi ya Moyo.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipokua akiwahutubia wananchi katika maadhimisho siku ya maradhi ya moyo Duniani huko Mnara wa kumbukumbu Kisonge.

Amesma wananchi waliowengi wanaathiriwa na maradhi hayo kutokana na kula mlo usiozingatia viwango ikiwa ni pamaoja na  kula vyakula vya uwanga kwa wingi bila ya kula matunda na mbogamboga ambazo zinasaidia kuzuwia matatizo ya afya.

“Tuna jukumu la kulinda afya zetu kwa kula vyakula vyenye afya na kuepuka kula vyakula visivyofaa ili tujiepusha na maradhi kwani kinga ni bora kuliko tiba” alisema Naibu Waziri.

Aidha amefahamisha kuwa maradhi  ya moyo yamekuwa yakiongeza idadi ya vifo siku hadi siku yakifuatiwa na maradhi ya sindikizo la juu la damu.

“Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa zinaonesha wazi kuwa mardhi hayo yapo, na yamekuwa yakiondoa uhai wa watu kwa kasi kubwa hivyo  ni wajibu wetu kufanya mazoezi na kurekebisha milo yetu,”alisema Naibu huyo.

Ameongeza kwa kusema kuwa maradhi ni kitu ambacho kila mtu anweza kukipata hivyo ipo haja kwa jamii kutowatenga wanaopata maradhi hayo kwa vile yanatibika na unaweza kujikinga kwa kuepuka mambo ambayo yanayosababisha maradhi hayo.

Hata hivyo amewashauri wataalamu na wale wote wanaohusika na mambo ya afya kushirikiana na vyombo vya habari kufanya vipindi maalum ambavyo vitaelezea sababu na namna ya kudhibiti ya maradhi hayo.

Akitoa takwimu ya maradhi hayo Dkt. Khamis Mustafa Khamis amefahamis kuwa zaidi ya wagonjwa 25 huongezeka kila mwakawqakiwemo watoto.

“Kumekuwa na na watoto 128 kwa mwaka 2022 ambapo 69 wanahitaji upasuaji” aliongezea Daktari huyo.

Hata hivyo Dkt Khamis ameeleza kuwa katika Hospiali ya Mnazi Mmoja  wamefanikiwa kuwawekea wagonjwa watano betri za moyo na ifikapo Novemba mwaka huu wanatarajia kuwawekea wagonjwa wengine.

Nae Afisa Uhusiano kutoka Taasisi ya watoto wenye maradhi ya moyo Zanzibar Arafa Kombo Sued ambae pia ni mgonjwa wa maradhi hayo amesema kuwa changamoto wanayokumbana nayo ni ukosefu wa vipimo na madawa jambo ambalo linawarejesha nyuma katika jitihada za kupambana na ugonjwa huo.

Aidha amefahamisha kuwa Tasisi yao wanapita katika jamii, maskulini, na hospitali na kutoa elimu juu ya ugonjwa huo kutokana na jamii kutokuwa na uelewa dhidi ya maradhi hayo.

Maadhimisho ya Siku ya magonjwa ya moyo Duniani hufanyika kila ifikapo September 29, ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni TUMIA MOYO KWA KILA MOYO.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.