Habari za Punde

Mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika Kati ya Timu ya Kipanga na Club Africain ya Tunisia Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu Hizo Zimetoka Sare ya 0-0

Wawakilishi wa Zanzibar katika mashindano yaKombe la Shirikisho Africa Timu ya Kipanga imeanza kwa sare ya bila ya magoli dhidi ya wapinzani wao Club Africain kutoka Nchini  Tunisia katika mchezo wa awali wa hatua ya pili ya michuano hiyo uliochezwa katika uwanja wa Amaan. 

Katika mchezo huo ambao ulichezwa majira ya saa 10:15 za jioni ulikuwa na ushindani kiasi ulihudhuriwa na mashabiki kiasi huku mashabiki wa timu ya Tunisia wakinogesha uwanja huo kwa shangwe zao uwanjani hapo na kuwasha fataki.

Aidha Tunisia watapaswa kujilaumu kutokana na kukosa penanti katika dakika ya  Tisa  ya mchezo huo iliyopigwa na Zouhaire Dhaouadi iliyosababishwa na kassim Ali aliemchezea rafu Ahmed Khalil.

Miamba hiyo iliendelea kushambuliana kwa zamu na kuzimaliza dakika 90 wakiwa hawajafungana.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.