Habari za Punde

Mradi wa Kuhamasisha Uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka Husika katika Kuboresha Elimu Wazinduliwa Pangani

MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalib Ringo akizundua mradi wa kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka husika katika kuboreshga Elimu na elimu Jumuishi kwenye Jamii wilayani Pangani kulia ni Mkurugenzi wa Tree Of hope Fortunata Manyeresa kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akifuatiwa na Mratibu wa Tree Of hope Goodluck Malilo
MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalib Ringo akipiga makofi mara baada ya akizundua mradi wa kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka husika katika kuboreshga Elimu na elimu Jumuishi kwenye Jamii wilayani Pangani kulia ni Mkurugenzi wa Tree Of hope Fortunata Manyeresa kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akifuatiwa na Mratibu wa Tree Of hope Goodluck Malilo
Mkurugenzi wa Tree Of hope Fortunata Manyeresa akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani Ghalib Ringo
  
              Mratibu wa Tree Of hope Goodluck Malilo akizungumza wakati wa uzinduzi huoNa 

Na.Oscar Assenga, PANGANI

MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalib Ringo amezindua rasmi mradi wa kuhamasisha uwajibikaji wa jamii na mamlaka husika katika kuboresha elimu  na elimu Jumuishi kwenye Jamii wilayani Pangani huku akieleza kwamba mradi huo utapata mafanikio makubwa na kuwa chachu kwenye jamii.a hiyo

Mkuu huyo wa wilaya aliyasema hayo  wakati akizindua mradi huo wa kuhamasisha uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha elimu na elimu jumuishi mjini Pangani 

Mradi huo unatekelezwa na Taasisi ya Tree of Hope kwa kupitia  ufadhili wa shirika la Foundation for Civil Society (FCS) ambapo umelenga kuongeza uwajibikaji wa mamlaka husika.

Alisema kwamba mradi huo umefika wilaya humo kwa wakati muafaka hulu wakiahaidi kutoa ushirikiano kwa kila hatua kwa kuhakikisha wanaufuatilia kutokana na mipango yao mizuri walionayo.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaeleza kwamba watakapofika kwenye vijiji watafute ratiba ya vikao vya kamati ya maendeleo ya Kata (WDC)  kwa Kata zote wapitishie elimu hiyo huko ili wataalamu na wajumbe wengine wanakwenda kwenye vijiji visivyo na mradi huo na kuweza kufikishiwa elimu hiyo.

Aidha alisema wakati wa mchakato wa kuchagua wajumbe wawaachie wananchi wachague wenyewe ili kuweza kupata watu ambao watakuwa chachu katika kutekeleza mradi huo ambao sana matumaini makubwa kuwa chachu ya mabadiliko kwenye elimu.

"Lakini niwaambieni kwamba kwenye maendeleo msijali masuala ya kisiasa angalieni huyu mtu anakubalika,anahamasa gani kwenye Jamii na sio kuangalia vyama wakati wa siasa utafika lakini leo tunapigana na maendeleo ya elimu "Alisema.

 Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope Fortunata Manyeresa alisema  kwamba wanashukuru kwa ushirikiano walioupata kutoka kwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Pangani na hivyo watahakikisha wanatekeleza mradi huo kwa tija na matokeo yake yalikuwa chachu kwenye Jamii.

Alisema kwamba kabla ya kufikiria kutekeleza mradi huo wilayani Handeni kwa kipindi cha miaka mitano ulikuwa na tija na mafanikio makubwa hivyo watahakikisha pia Pangani wanatakeleza vema zaidi na hivyo kuendelea kumshawishi mfadhili endelee kupeleka mradi hapa.

Naye kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange alisema kwamba anaamini timu hiyo italeta manufaa kwenye changamoto za elimu katika wilaya ya Pangani.

Hata hivyo Mratibu wa Taasisi ya Tree of Hope Goodluck Malilo alisema mradi huo ni mpya katika wilaya hiyo na unatekelezwa katika vijiji vinne vilivyopo Kata za Mkalamo,Mikunguni,Kipumbwi,na Kijiji cha Ubangaa.

Alisema kwamba wanatarajia matokeo makubwa mawili ambao ni mradi wa miezi nane ambapo utolewaji wa huduma za elimu Bora na Jumuishi za elimu kwenye vijiji vyote vinne wanavyotekeleza mradi huo watafikiwa na lengo la kuwajengea uwezo kwa wahusika viongozi na wananchi kwa njia ya midahalo na mikutano ya kimkakati ya kwenda kutatua changamoto au vikwazo vinavyopelekea kufifisha utolewaji wa huduma Bora za elimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.