Habari za Punde

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa CZECH Awasili Nchini kwa Ziara

Balozi wa Tanzania nchi Ujerumani ambaye pia anawakilisha Jamhuri ya Czech, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa amewasili nchi leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 2 hadi 4 Oktoba 2022.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Tlapa amepokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme na Balozi wa Tanzania nchi Ujerumani ambaye pia anawakilisha Jamhuri ya Czech, Mhe. Dkt. Abdallah Possi.

Akiwa nchini, Mhe. Tlapa kwa nyakati tofauti, atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Nchi-Tamisemi,  Waziri wa Afya,  Waziri wa Viwanda na Biashara, pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) pamoja na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Hospitali ya Jeshi la Wananchi (JWTZ).  

Tanzania na Czech zimekuwa zikishirikiana katika sekta za elimu,utamaduni, afya, biashara na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.