Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azindua Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 na Kutangaza idadi ya Watanzania milioni 61,741,120.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua Kitabu cha Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 mara baada ya kukizindua katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 31 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akinyanyua Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 31 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Vitabu vya Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na Kitabu cha Muongozo wa Kitaifa wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuzindua Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi katika Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 31 Oktoba, 2022. Katika uzinduzi huo, Mhe. Rais alitangaza idadi ya Watanzania kuwa ni Milioni 61,741,120 ambapo Wanaume ni 30,053,130 na Wanawake ni 31,687,990.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma waliofika kushuhudia uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, tarehe 31 Oktoba, 2022.
Sehemu ya viongozi pamoja na Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 31 Oktoba, 2022.
Makarani wa Sensa wakiwa katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kuhudhuria sherehe za uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa na Makazi ya mwaka 2022.
Vikundi mbalimbali vya Ngoma za asili na kwaya vikitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 31 Oktoba, 2022.
 Vikundi mbalimbali vya Ngoma za asili na kwaya vikitumbuiza katika sherehe za uzinduzi wa Matokeo ya Mwanzo ya Sensa ya Watu na Makazi katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma tarehe 31 Oktoba, 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.