Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amekutana na Kuzungumza na Watanzania Wanaoishi Nchini Oman Diaspora

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapoinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi na Kiongozi wa Diaspora wa Tanzania Nchini Oman, baada ya kumaliza mazungumzo yake na Wanadiaspora wakati wa ziara yake Nchini Oman.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Diaspora wa Tanzania Nchini Oman wakati wa ziara yake Nchini Oman. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi,  amekutana na Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman maarufu Diaspora. 

Katika mkutano huo Dk. Mwinyi aliwaeleza wana Diaspora hao lengo la ziara yake nchini Oman,  kwanza ni kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya  Tanzania Zanzibar  hasa na Oman na pia kutafuta fursa za biashara zitakazojenga uchumi. 

Aliwafahamisha hali ya utulivu ilivyo Zanzibar na kuwataka kuwekeza kwani ni wakati mzuri sasa kufanya hivyo. 

Pia aliwapo somo kuhusu sera ya uchumi wa buluu na akainisha mambo matano serikali inavyojikita katika kuingia katika sera hiyo. 

Aliyataja mambo hayo kuwa ni Utalii, uimarishaji bandari kubwa kwa ujenzi wa Bandari kubwa eneo la Mangapwani,  

uchimbaji wa mafuta na gesi na kubainisha , na usafiri wa baharini. 

Rais Dk. Mwinyi alisema yote hayo yaende vizuri ni lazima juwe na umeme wa uhakika, maji, barabara nzuri na mfumo mzuri wa IT. 

Mhe.Rais  Dk Hussein Ali Mwinyi pia aliwashukuru wana Diaspora wanaojitolea kwa misaada mbalimbali ya kijamii. 

Dk Hussein Ali Mwinyi na ujumbe wake watamaliza ziara ya Oman kesho ijumaa 14-10-2022. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.