Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali AbdulGulam Hussein amewasisitiza wanafunzi wa Kidato cha nne (4) kusoma kwa jitihada wakitambua Taifa kuwa linawategemea.
Ameyasema hayo leo tarehe 17 Oktoba, 2022 wakati alipokabidhi vyakula na vifaa vya kusomea vilivyochangiwa na Taasisi ya ROZAC Ltd kwa Skuli ya Jang'ombe na Kidongo Chekundu.
Aidha Naibu Waziri amewapongeza ROZAC kwa kutoa mchango katika Elimu ya Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kusaidia maendeleo ya Zanzibar.
Mhe Abdulgulam Amesema ili Elimu ipatikane kwa kila mwanachi ipo haja ya kushirikiana na kila mdau kwa namna yake ili kuhakikisha Elimu Zanzibar unapatikana Katika kiwango Bora na miundombinu mizuri.
Amesema utoaji wa Elimu unahitaji mashirikiano baina ya wahisani na wasimamizi wa sekta hiyo ili kufikia malengo ya utoaji wa Elimu katika kiwango Bora.
Aidha amewasisitiza kusema kuwa suala la uboreshaji wa Elimu nchini ni suala la kila mtu kwa kushirikiana na sekta husika.
amesema suala la kutafuta Elimu ni haki ya lazima kwa kila mwanachi hivyo zinapotokea fursa za kuboresha sekta hiyo ni vyema kuzitumia ipasavo ili kufikia malengo kuwa na taifa lenye wasomo wa taaluma mbalimbali.
Mapema mkuu wa kitengo cha elimu ya juu bi Aida Juma Moulid amesema ili Wanafunzi waendelee kupata matokeo mazur ipo haja kwa wizara kuendelea kuthamini fursa zinazotolewa na wadau mbalimbali wa Elimu nchini.
Nae Mkurugenzi wa taasisi ya Rozac Bi Sabra Abdallah Khamis imesema itaendelea kushirikiana na wizara ya Elimu kuhakikisha wanawapa hamasa Wanafunzi kwa kuwapa zawadi pale wanapopata matokeo mazuri na kuwafanya wengine nao waongeze jitihada zaidi.
Katika hafla hiyo vifaa mbalimbali vilikabidhiwa ikiwemo mchele mafuta, karatasi za mazoezi na chumvi.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali AbdulGulam Hussein akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhiwa vyakula kwa Wanafunzi wanaojiandaa na Mitihani yao ya Kidatu cha Nne wa Skuli ya Jangombe na Kidongochekundu Unguja 
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali AbdulGulam Hussein akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi na Viongozi RAZAC, baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhiwa vyakula kwa Wanafunzi wanaojiandaa na Mitihani yao ya Kidatu cha Nne wa Skuli ya Jangombe na Kidongochekundu Unguja
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali AbdulGulam Hussein amewasisitiza wanafunzi wa Kidato cha nne (4) kusoma kwa jitihada wakitambua Taifa kuwa linawategemea.
Ameyasema hayo wakati alipokabidhi vyakula na vifaa vya kusomea vilivyochangiwa na Taasisi ya ROZAC Ltd kwa Skuli ya Jang'ombe na Kidongo Chekundu.
Aidha Naibu Waziri amewapongeza ROZAC kwa kutoa mchango katika Elimu ya Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kusaidia maendeleo ya Zanzibar.
Mhe Abdulgulam Amesema ili Elimu ipatikane kwa kila mwanachi ipo haja ya kushirikiana na kila mdau kwa namna yake ili kuhakikisha Elimu Zanzibar unapatikana Katika kiwango Bora na miundombinu mizuri.
Amesema utoaji wa Elimu unahitaji mashirikiano baina ya wahisani na wasimamizi wa sekta hiyo ili kufikia malengo ya utoaji wa Elimu katika kiwango Bora.
Aidha amewasisitiza kusema kuwa suala la uboreshaji wa Elimu nchini ni suala la kila mtu kwa kushirikiana na sekta husika.
amesema suala la kutafuta Elimu ni haki ya lazima kwa kila mwanachi hivyo zinapotokea fursa za kuboresha sekta hiyo ni vyema kuzitumia ipasavo ili kufikia malengo kuwa na taifa lenye wasomo wa taaluma mbalimbali.
Mapema mkuu wa kitengo cha elimu ya juu bi Aida Juma Moulid amesema ili Wanafunzi waendelee kupata matokeo mazur ipo haja kwa wizara kuendelea kuthamini fursa zinazotolewa na wadau mbalimbali wa Elimu nchini.
Nae Mkurugenzi wa taasisi ya Rozac Bi Sabra Abdallah Khamis imesema itaendelea kushirikiana na wizara ya Elimu kuhakikisha wanawapa hamasa Wanafunzi kwa kuwapa zawadi pale wanapopata matokeo mazuri na kuwafanya wengine nao waongeze jitihada zaidi.
Katika hafla hiyo vifaa mbalimbali vilikabidhiwa ikiwemo mchele mafuta, karatasi za mazoezi na chumvi.
No comments:
Post a Comment