Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa
pili wa kumuenzi Marehemu Maalim Seif
uliofanyika hoteli ya Golden Tulip leo tarehe 22.10.2022 . Mkutano huo
umeandaliwa na Maalim Seif Foundation na kuwashirikisha wataalamu , wanasiasa ,
wanadipmomasia na viongozi mbali mbali.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa
pili wa kumuenzi Marehemu Maalimu Seif Sharif Hamad wakimsikiliza Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, alipozungumza katika
ufunguzi wa mkutano wa pili wa kumuenzi Marehemu Maalim Seif uliofanyika hoteli ya Golden Tulip leo tarehe
22.10.2022 . Mkutano huo umeandaliwa na Maalim Seif Foundation na
kuwashirikisha wataalamu , wanasiasa , wanadipmomasia na viongozi mbali mbali.
Picha Na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Kitengo cha habari.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba wakati nchi inaelekea katika mjadala wa Mageuzi makubwa ya sekta ya elimu ni wajibu kwa Wazanzibari kuwa na tafakuri ya kina juu ya umuhimu wa suala hilo na namna kulifanikisha kwake.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko
hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki mjini Zanzibar, alipofungua mkutano wa pili
wa kumuenzi Maalimu Seif Sharif Hamad ulioandaliwa na Maalim Seif Faoundation na kuwashirkisha wanataalama, wanasiasa, na
wanadiplomasia kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mhe. Makamu amesema kwamba hatua
hiyo ni muhimu katika jitihada za pamoja za kujenga khatima njema ya
Zanzibar kielemu kwa kuzalisha vijana
wenye maarifa na uwerevu wa kitaaluma hasa kwa vile taifa imara linategemea
sana kizazi makini kilichotayarishwa kukabiliana na changamoto zilizopo na
zijazo.
Amefahahamisha kwamba hali hiyo ni
lazima kwenda sambamba na kuwepo
maridhiano ya kweli, amani na utulivu nchini na kuwepo jitihada kubwa za kutajenga uchumi imara na kuleta maendeleo ya kweli nchini.
Aidha Mhe. Othman amesema kwamba
hili hiyo nilazima pia kuziweka katika tafakuri na tathimini sahihi rasilimali
za aina mbali mbali zilizopo nchini katika kuijenga Zanzibar kuwa imara zaidi kupitia elimu itakayotolewa.
Amesema kwamba kuwepo Zanzibar yenye uchumi imara ni muhimu
katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazokwamisha maendeleo ya nchi.
Mhe. Othman amesema kwamba katika kukabiliana na hali bora ya
kuwatayarisha vijana kielimu ni lazima kwa serikali kutengeneza na kuwepo
sera na uendeshaji bora wa sekta hiyo ya
belimu unaosaidiwa na usimamizi bora
sambamba na kuwepo muono sahihi katika
uongozi wa ngazi mbali mbali.
Aidha Mhe Othman amesema
kumtayarisha mtoto kuwa mwerevu kielimu kutasaidiwa sana na kuwepo makuzi na malezi
bora kwa kuzingatia mazingira anayoishi
ikiwemo usomeshaji na kuwepo na
kutumika mitaala bora huku mwalimu
akipewa umuhimu wa kipekee kutokana na uwezo wake wa kumsaidia mwanafunzi kujifunza.
Mhe. Othman amesema kwamba nchi ni
lazima ijitahidi kukubuni mbinu tofauti zitakazosaidia
kuhakikisha kwamba sekta ya elimu
inazalisha vijana werevu watakaokwenda
samabamba na mahitaji ya sasa nay a baadaye yanaongozwa na mabadiliko ya
sayansi na teknolojia kwa manufaa ya taifa
na kwamba jambo hilo linawezekana kufikiwa ingawa njia za kufikia
zinaweza kutafautiana.
Naye Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Issa
Shivji, akiwasilisha mada kuhusu uhuru wa elimu kama msingi wa Demokrasia ,
amasema kwamba huwezi kuwa na elimu bora bila kwepo walimu bora wanaoweza
kutengeneza vipaji kwa vijana.
Amesema kwamba walimu ndio wenye
uwezo na upeo sahihi wa kukuza vipaji vya wanataaluma na kuzalisha wasomi bora
wanaojimani katika kuchangia vyema maendeleo ya taifa lao.
Professa Shevji amesema kwamba
wanafunzi wa namna hiyo ndio wenye uwezo wa kujadili na kudadisi mawazo mbali mbali yaliyopo na kutoa mbadala yatakayosaidia vijana kuweza kuchangia
upeo wa maendeleo ya nchi yao.
Nao baadhi ya washiriki katika
Mkutano huo wamesema kwamba katika kuhakikisha maendeleo bora ya elimu nimuhimu
kujadili , kupanga na kuamua kuanzisha mifuko mbali mbali itakayosaida kuwa
miundombinu ya kukuza maendeleo ya sekta
ya elimu ili kupata vijana wenye uwezo mkubwa kitaaluma.
Mkutano huo wa Siku mbili ambao ni
wa pili umetayarishwa na Maalimu Seif Foundation, na umewakutanisha
wananasiasa, wataalamu , wanadiplomasia na wananchi mbali mbali utatajidili
mada kadhaa ikiwa ni hatua ya kuenzi Fikra za Marehemu maalum seif Sharif
kutokana na mchango wake mkubwa katika kuwaleta wananchi wa Zanzibar na
Tanzania kwa jumla pamoja, kuhubiri
amani na mshikamano pamoja na kuchangia ukuaji
wa demokrasia na haki za binaadamu nchini.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo cha Habari leo tarehe 22.10.2022.
No comments:
Post a Comment