Habari za Punde

UVCCM Iringa Vijijini Wamuunga Mkono Rais Mhe.Samia Ujenzi wa Madarasa kwa Vitendo

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Elia kidavile akiwa anashusha kokoto katika shule ya sekondari ya William Lukuvi katika kata ya Ilolo Mpya ikiwa ni kuonyesha namna gani wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Elia kidavile akipanda mti katika shule ya sekondari ya William Lukuvi katika kata ya Ilolo Mpya ikiwa ni kuonyesha namna gani wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu

Na Fredy Mgunda, Iringa.

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana ya Chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Iringa Vijijini yaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kujitolea kuchangia kokoto mchanga na nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi katika shule ya sekondari William Lukuvi ikiwa ni sehemu ya utekelezwaji wa ilani ya CCM katika kuboresha elimu nchini 

Akizungumza na vijana wa jumuiya hiyo kata ya Ilolo Mpya Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa vijijini Elia kidavile alisema kuwa vijana wa chama hicho ni lazima kumuunga mkono Rais Samia kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa watanzania.

Kidavile alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imeamua kuwapunguzi michango wazazi kwa kutoka fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu katika shule mbalimbali hapa nchi hata vijana wa chama cha mapinduzi inatakiwa kuonyesha mfano kwa kumuunga mkono Rais.

Alisema kuwa zamani wazazi walikuwa na jukumu kubwa la kuchangia michango mikubwa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa,ofisi na nyumba za walimu lakini kwa sasa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imepunguza adha hiyo kwa kuamua kujenga vyumba vya madarasa kila mwaka na kuwaacha wananchi waendelee na shughuli nyingine za kimaendeleo.

Kidavile aliwapongeza vijana wa chama cha mapinduzi kata ya Ilolo Mpya kwa kujitolea kuchangia kokoto,mchanga na nguvu kazi katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu katika shule ya sekondari William Lukuvi na kuwaomba vijana wengine wa chama hicho kuiga mfano huo.

Aloice Mkongo na anord masagari ni vijana wa jumuiya hiyo ya  UVCCM wilaya ya Iringa vijijini wameamua kujitolea kuchangia shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari William Lukuvi  kutoka na kazi nzuri ya kimaendeleo ambayo imekuwa unafanywa na Rais Samia.

Kwa upande wake kaimu afisa Tarafa ya Pawaga Emmanuel Ngabuji alisema kuwa Umoja wa Vijana Kata ya Ilolo mpya umewasilisha kwa vitendo shukrani zao kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo hayo

Ngabuji alisema kuwa zaidi ya Milioni mia sita (600,000,000) zimetolewa kwenye tarafa ya Pawaga kwa ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali za sekondari ambapo imewapunguzia wananchi kuchangia kwenye ujenzi wa madarasa hayo.


Alisema kuwa vijana wanatakiwa kuipenda nchi yao na viongozi wanaowaongoza kwa kuwa wamekuwa wakionyesha njia ya kuleta maendeleo kwa wananchi wote.

Ngabuji alimazia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo kwa watanzania na kuomba watanzania waendelee kumuunga mkono.

Akitoa neno la shukrani kwa vijana hao waliojitolea katika  kuchangia ujenzi wa madarasa na Ofisi Kaimu mkuu wa shule ya Sekondari Wiliam lukuvi Abisai Ugi amesema hatua hiyo imesaidia pakubwa kufanikisha mradi huo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.