Habari za Punde

Waziri Mhe.Mchengerwa Ashuhudia Michuano ya UEFA Europa Nchini Uturuki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa jana Oktoba 6, 2022 amehudhuria Mashindano ya UEFA EUROPA League kwa mualiko maalum kutoka kwa Rais wa Klabu ya Fenerbahce Ali Koc.

Waziri Mchengerwa alipata wasaa wa kushuhudia mechi kati ya Fenerbahce na AEK Larnaca, mechi iliyochezwa katika uwanja wa klabu hiyo nchini Uturuki.

Katika mechi hiyo timu ya Fenerbahce wameibuka washindi dhidi ya AEK kwa goli 1-0.

Akizungumza mara baada ya mechi Rais huyo ameahidi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika kuinua sekta ya michezo nchini.

Waziri Mchengerwa aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Lt. Gen. Yacoub Mohamed.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.