Habari za Punde

TANESCO Kanda ya Kaskazini Waeleza Mikakati Upatikanaji wa Umeme wa Uhakika

Mkurugenzi wa Tanesco Kanda ya Kaskazini Mhandisi Fedgrace Shuma kulia akiwakabidhi tuzo na cheti kwa uongozi wa Kiwanda cha PPTL Jijini Tanga ikiwa ni kama wateja wakubwa wa Shirika hilo ikiwa ni wiki ya mteja duniani
Mkurugenzi wa Tanesco Kanda ya Kaskazini Mhandisi Fedgrace Shuma kulia akiwakabidhi tuzo na cheti kwa uongozi wa Kiwanda cha Maweni Limestone Jijini Tanga ikiwa ni kama wateja wakubwa wa shirika hilo ikiwa ni wiki ya mteja duniani
Mkurugenzi wa Tanesco Kanda ya Kaskazini Mhandisi Fedgrace Shuma kulia akiwakabidhi tuzo na cheti kwa uongozi wa Kiwanda cha Tanga Cement  Jijini Tanga ikiwa ni kama wateja wakubwa wa shirika hilo ikiwa ni wiki ya mteja duniani

Na Oscar Assenga,TANGA.                                                                                                                        

SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) Kanda ya Kaskazini wameeleza mipango kabambe ya kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika unaotokana na uboreshwaji wa  miundombinu iliyopo lengo likiwa ni kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo wakati wote.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Tanesco Kanda ya Kaskazini Mhandisi Fedgrace Shuma wakati wa ziara ya kuwatembelea wateja wakubwa mkoani Tanga wenye viwanda ikiwa ni wiki ya mteja ambapo alisema mkakati huo utakapokamilika utawezesha wananchi kupata umeme wa uhakika muda wote.

Katika ziara hiyo Mkurugenzi huyo alipata ya kutembelea wateja wakubwa kupitia viwanda vya Tanga Cement,Maweni Limestone na PPTL kusikiliza maoni yao kuhusu huduma ambazo wanazipata kwenye Shirika hilo ikiwemo kuwaeleza mipango yao ya muda mfupi na mrefu.

Sambamba na hilo lakini pia walitoa ushauri ikiwa kuna tatizo la umeme wawe wanatoa taarifa kwa wakati na kuwashukuru kwamba wamekuwa wakipewa taarifa na hivyo kuona namna ya kukabiliana nazo.

Mkurugenzi huyo wa Kanda ya Kaskazini alisema lengo la kuwatembelea wateja wakubwa wenye viwanda na wadogo ni kuwasikiliza kujua maoni pia kama kuna maboresho wanawashauri na baadae kuzifanyia kazi ili ziweze kuondosha changamoto zilizokuwepo awali.

"Kwa sasa Shirika kuna mambo mengi mazuri ikiwemo mfumo wa Nikonect kwa akili ya kuombea umeme Tanesco mteja hapaswi kufika kwetu anaingia kwenye simu yake na kupata huduma ya umeme". Alisema.

Katika ziara hiyo ya Mkurugenzi waliwakabidhi pia  trophy kwa kutambua mchango wao muhimu kwenye Shirika hilo kwa kuwa wamekuwa wakitumia huduma zao hivyo kupitia siku ya wateja duniani wakaona wathamini mchango wao.

"Lakini ushauri wao tutakwenda kuufanyia kazi hususani katika suala la miundombunu iliyopo inaendelea kufanyiwa maboresho ili mteja aweze kupata huduma masaa yote na kwa maana umeme usikatike kutokana na changamotomo zao bali mteja aamue kuzima kiwanda mwenywe afanye matengenezo"Alisema

Naye kwa upande wake Fundi wa Umeme katika Kiwanda cha PPTL kilichopo Duga Jijini Tanga  Saidi Msuya aliwashukuru Tanesco kwa utaratibu waliouweka wa kukutana  a wateja wao ili kuweza kubaini changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.

Alisema kwamba walichokiomba kuwepo na utaratibu wanapouliza jambo waweze kupatiwa majibu kwa haraka ili kuweza kujipanga na iwapo umeme nitakuwepo au la kuwawezesha kupanga ratiba zao za kazini.

Hata hivyo alisema mikakati ya Shirika hilo ni mizuri hasa kwa mpango wake wa kufanyia maboresho ya miundombinu ambayo utawezesha kuondosha vikwazo hivyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.