MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amewataka Vijana nchini kuzitumia vyema fursa za kutengeneza ajira zinazoanzishwa na serikali ili waweze kufikia ndoto zao za kuwa na ajira za uhakika kwa maendeleo ya na taifa kwa jumla.
Mhe. Othman ameyasema hayo katika
Ukumbi wa Dk Ali Mohammed Shen huko Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar ( SUZA)
alipozungumza katika Tamasha la Kongamano la vijana la Ndoto ajira
lilowakutanisha vijana kutoka ndani nan je ya Tanzania.
Mhe. Makamu amefahamisha kwamba
ukosefu wa ajira kwa vijana ni moja ya
changamaoto kubwa za kijamii
inayozikabili nchi nyingi duniani na zaidi
barani Afrika na kwa kiasi kikbwa inachangiwa na mitazamo ya vijana kutegemea
kuajiriwa serikali pekee.
Amesema Tamasha hilo la Ndoto-
Ajira ni fursa kubwa kwa vijana wa Afrika Mashariki kujionea namna
wanavyowasilisha mawazo yao na ubunifu walionao katika Nyanja za biashara na
sekta ya uchumi wa bluu ili kutimiza malengo yao ya kujiajiri
na kuondokana na mawazo ya kuajiriwa serikali kama fursa pekee ya ajira.
Amefahamisha kwamba serikali kupitia Ofisi ya Rais, Kazi , Uchumi na
uwezeshaji wananchi kiuchumi imeunda chombo cha Wakala wa Uwezeshaji wananchi
kiuchumi ili kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao kwa kuweza kupatiwa
mafunzo ya ujasiriamali , mikopo na
kutafutiwa masoko kwa bidhaa wanazozalisha na kusaidia kukuza pato kwa vijana.
Hivyo Mhe. Othman amesema kwamba
serikali kupitria Taasisi zake na kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo
imeandaa program maalum za kuwawezesha vijana kwa kuwakuza kiujizi kupitia
skuli na vyuo vyua Ufundi , vituo vya uwezeshaji ili waweze kuingia katika soko
la ajira na kujikwamua kiuchumi na kupunguza tatizo la ajira.
Amefahamisha kwamba kufanya hivyo
ni jitihada maalumu za kutafuta
suluhisho muhimu kwa tatizo la ajira kwa
kuwaandaa vyema vijana wenye elimu
sahihi , ujuzi na maarifa ya kazi kwa kuweza kujiajiri na kutimiza ndo yao ya
ajira.
Mhe. Makamu amesema kwamba hali
hiyo ni kutokana na ukweli kwamba serikali inafahamu vyema kundi kubwa la
vijana linapaswa kuangaliwa vyema kwa matazamo wa aina yake kwa lengo la
kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kukuza uchumi na kueleta
maendeleo nchini.
Amefahamisha kwamba serikali
inafanya hivyo kwa kutambua mchango mkubwa wa viajana kwa maendeleo ya taifa
hivyo itaendelea kuimarisha uwezo wao katika Nyanja za kujumuisha elimu,
sayansi na Teknolojia, ubunifu, uchumi, Sanaa, utamaduni na michezo ili kuenua ustawi wa maendeleo ya vijana kwa
sasa na baadae.
Aidha aliwataka vijana kutambua
kwamba muda ni thamani kubwa katika masisha ya mwanadamu na kwamba wanapaswa
kuutumia vyema kwa kujitahidi kujiaanda
katika kutafuta mafanikio yao ya kiuchumi na kimaendeleo bila kukata tamaa.
Naye Waziri wa Nchi Afisi ya Rais ,
Kazi , Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Suraga, amesema kwamba ukosefu
wa ajira kwa vijana ni kilio cha muda mrefu na kwamba Ndoto- Ajira wamekuja na
mtazamo mpya kuhusu changamoto hiyo kwa vijana.
Amesema kwamba vijana wanaweza
kuzitumia fursa mbali mbali zinazoanzishwa katika jitihada za kuwa wabunifu ,
kutumia elimu na maarifa wanayopatiwa na
hatimae waweze kupata mafanikio katika jitihada zao za kuleta maendeleo.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo cha Habari leotarehe 19.11.2022.
No comments:
Post a Comment