Habari za Punde

Wanahabari watembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Marekebisho ya tabia na miradi ya Ujasiriamali Kidimni

Kamishna tiba kinga na marekebisho ya Tiba  Juma Zidikheir akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa ujenzi wa kituo cha Marekebisho ya tabia na miradi ya Ujasiriamali Kidimni Wilaya ya kati Zanzibar (kulia) Khamis  Vuai Rajab kutoka Kamisheni utawala na Mipango na Raya Hamad Mwandishi muandamizi kutoka Afisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar.
Kamishna wa Kinga na marekebisho ya Tiba  Juma Zidikheir  akiwaonyesha waandishi ramani ya majengo yanayoendelea kujengwa katika kituo cha Marekebisho ya tabia na miradi ya Ujasiriamali Kidimni Wilaya ya kati Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe na waandishi wakielekea katika yanayoendelea kujengwa katika kituo cha Marekebisho ya tabia na miradi ya Ujasiriamali Kidimni Wilaya ya kati Zanzibar.
Daktari dhamana wa kituo cha Marekebisho ya tabia na miradi ya Ujasiriamali Abdulrahman Abdulla akiwapa maelezo waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi anavyofundisha wakati anapokuwa darasani watu wanaorekebishwa tabia.

Kamishina tiba kinga na marekebisho ya tiba  Juma Zidikheir akiwaonyesha mitambo baadhi ya waandishi wahabari itakayotumika kwa ajili ya kuoshea gari.
Kamishna  wa Tiba Kinga na marekebisho ya Tiba  Juma Zidikheir akizungumza na waandishi wa habari akionyesha kompyuta itakayotumika kwaajili ya kuonyeha vifaa wakati  inapochunguzwa mara wakati wa kuwasilishwa eneo hilo.

Picha na Miza Othman  - Maelezo Zanzibar.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.