Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akimkabidhi mama mjamzito mojawapo ya mtungi wa gesi kati ya mitungi 100 aliyogawa kwa wanawake wajawazito kwa ajili ya kupunguza shughuli nzito za kutafuta nishati mbadala katika hafla fupi iliyofanyika Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza leo.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akiwa ameambatana na Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Magu amegawa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 14 kwa Hospitali ya Wilaya ya Magu pamoja na mitungi ya gesi 100 kwa wanawake wajawazito.
Akizungumza
leo katika hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi
14,575,000 na mitungi ya gesi 100 kwenye Hospitali ya Magu, Mhe. Masanja
amesema vifaa hivyo vimetokana na mchango wake binafsi pamoja na mchango wa
Doris Mollel Foundation.
Amefafanua
kuwa vifaa tiba hivyo vitasaidia kuokoa maisha ya watoto waliozaliwa njiti na
pia mitungi ya gesi itasaidia wanawake wajawazito kupunguza shughuli nzito za
kutafuta nishati mbadala.
Mhe.
Masanja amewaasa wanawake wajawazito kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kujua
maendeleo ya mtoto anapokuwa tumboni.
Aidha,
Mhe. Masanja amewataka wanawake wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kumuunga
mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
kwa jitihada anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Magu Dkt.Maria Kapinga amesema vifaa hivyo
vilivyotolewa na Naibu Waziri Masanja vitasaidia kunusuru maisha ya watoto
wanaozaliwa kabla ya muda ( njiti).
No comments:
Post a Comment