Habari za Punde

Serikali Inafanya Manoresho Makubwa Hospitali ya Muhimbili --MAJALIWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza na wagonjwa wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, Disemba 23, 2022
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akitazama mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) wakati alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam, Disemba 13, 2022.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi wakati alipotembelea Hospitali hiyo jijini Dar es salaam, Disemba 23, 2022.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimpa pole  Jackline Meena anayemuuguza mtoto  Bryton Mbikilwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam wakati alipotemblea Taasisi hiyo  Disemba 23, 2022
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati alipoitembelea hospitali hiyo jijini Dar es salaam, Disemba 23, 2022.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanya maboresho makubwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Amesema kuwa katika kutimiza hilo hivi karibuni imetoa fedha kwa ajili kununua vifaa vya kisasa ikiwemo MRI ambayo inaweza kumpima mgonjwa hata akiwa na chuma mwilini.

Sambamba na huduma hizi nzuri zinazotolewa na wataalam wetu kwa moyo mkubwa Serikali inaendelea kufanya maboresho makubwa katika hospitali yetu ya Taifa ili iendelee kutoa huduma bora na za kisasa zaidi.”

Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Desemba 23, 2022) baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo na kuzungumza na wagonjwa na wauguzi ambao wamemueleza kuwa huduma zinazotolewa hospitali hapo zinaridhisha.

Pia, Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na huduma za matibabu zinazotolewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na amewapongeza watendaji wa hospitali hiyo kwa kuendelea kuwahudumia wagonjwa kwa weledi na ufanisi mkubwa.

Akizungumzia suala la gharama kubwa za matibabu ambalo limelalamikiwa na wananchi wengi wanaouguza ndugu zao, Waziri Mkuu amesema mpango wa bima ya afya kwa wote unakwenda kumaliza changamoto hiyo.

Pia, Waziri Mkuu amewataka Watanzania ambao wanashindwa kumudu baadhi ya huduma za matibabu wawasilishe masuala yao katika ofisi ya Ustawi wa Jamii zilizopo kwenye hosptali husika na watapewa maelekezo ya kufuata ili wapate msamaha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Mohammed Janabi amewasisitiza wagonjwa wote ambao hawana uwezo wa kulipia huduma hizo mbalimbali zitolewazo hospitalini hapo wafuate taratibu watahudumiwa. “Kila mwezi hospitali inatoa msamaha wa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa wasiokuwa na uwezo.”

Wakizungumzia kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wanaouguza ndugu zao katika hospitali hiyo wamesema kuwa huduma zitolewazo ni nzuri na hakuna anayeombwa rushwa ila changamoto waliyonayo ni kwamba matibabu yanatolewa kwa gharama kubwa.

Miongoni mwa wanaoguza ndugu zao Bibi Abia Mjule alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa maboreshi ya huduma ikiwemo misamaha ya matibabu inayotolewa kwa wagonjwa wasiokuwa na uwezo.

Mjukuu wangu alilazwa Novemba 23 mwaka huu na amefanyiwa upasuaji wa moyo ambao gharama yake ilikuwa shilingi milioni 4.26, naishukuru Serikali baada ya kuomba kupunguziwa ilikubali na nikalipa nusu na nusu ililipwa na Serikali.”

(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

IJUMAA, DESEMBA 23, 2022.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.