Habari za Punde

KVZ Mabingwa Kombe la Mapinduzi Cup 2023 Netiboli Kwa Kuifunga Zimamoto 50-39.

Na Maulid Yussuf WMJJWW  Zanzibar

Timu ya Netball ya kikosi cha KVZ imeibuka kidedea katika Fainali za mashindano ya Netbal  Mapinduzi Cup 2023 ulichozwa katika Viawanja vya Gymkhana, Mjini Unguja hapo jana.

Mchezo huo wa Fainali umeuhusisha timu za Wanawake kutoka Vikosi vya KVZ na Zimamoto, ambapo KVZ imefanikiwa  kuichapa Zimamoto magoli 50 kwa 39.

Mpaka kufikia mzunguuko wa tatu wa mapumziko katika mchezo huo, KVZ ilionekana kuongoza kwa magoli 37 dhidi ya Zimamoto kwa kuwa na magoli 27.

Akizubgumza baada ya kumalizika mchezo huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma amewapongeza washindi pamoja na washiriki wote wa mchezo huo wa netball kwa kushiriki mchezo huo kwa mashirikiano mazuri pamoja na nidhamu ya hali ya juu.

Amesema michezo ni Afya, michezo pia inajenga mashirikiano na nidhamu, hivyo amewataka kuendeleza mashirikiano hayo pamoja na nidhamu katika sehemu nyengine, ili kufikia malengo yao.

Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi Makini wa Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi umeahidi kuweka kipaumbele katika michezo katika bajeti yake ya 2023-2024, kwa kuendelea kujenga viwanja vya michezo vya kisasa kwa lengo la kuimarisha michezo hapa nchini.

Hivyo amesema changamoto yao ya ukosefu wa viwanja vya kisasa naamini Dkt Hussein ataitatua, na kuwaonba uwa na uvumilivu katika kufikia malengo hyo.

Pia Mhe Riziki ametumia fursa hiyo, kuwaomba wakuu wa Vikosi hivyo uangalia uwezekano wa  kuwapandisha vyeo wachezaji wake hasa Wanawake, kwani wamekuwa wakiwaletea sifa kubwa vikosi vyao katika michezo.

Nae Katibu wa Chama cha Netball Zanzibar CHANEZA ndugu Said Ali Mansab amesema mashindano hayo kikawaida hufanyika kila mwaka ikiwa lengo ni kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, kuwa ni chachu ya kuinua  michezo Zanzibar pamoja na kuinua vipaji vya vijana katika kujipatia ajira kimichezo.

Amesema mashindano hayo  ya Netball Mapinduzi Cup, yalianza tarehe 4 January mwaka 2023 ambapo jumla ya timu saba zilishiriki, ikwemo KVZ, Zimamoto, Bandari, Mafunzo, Afya, Ztalent na timu ya Worious.

Katika mchezo huo wa Fainali,  KVZ ilijinyakulia Kombe la ushindi, fedha taslim shilingi milioni moja, pamoja na medali, huku zimamoto iliyoshika nafasi ya pili ilipata medali na fedha taslim shilingi laki tano na mshindi wa tatu timu ya Bandari ilijinyakulia kombe la nidhamu pamoja na medali.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.