Na.Mwandishi wa OMKR.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Maoud Othman, amesema kwamba juhudi kubwa zinazofanywa na
serikali katika uwekezaji wa kuweka miundombinu kwenye miradi ya maendeleo
lazima viongozi na wananchi kuweka mikati imara ya kuitunza ili miradi
inayoanzishwa iweze kuwa endelevu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman ameeleza hayo alipohotubia katika hafla ya
uwekaji wa jiwe la msingi la tangi la maji safi na salama huko Masinginbi Wilaya
ya Magharib ‘A’ Unguja ikiwa ni shamra shamra za kutimia miaka 59 tokea
kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964.
Amefahamisha kwamba, hatua ya
kuwepo miradi ya aina hiyo ni jitihada za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kulipa umuhimu mkubwa suala la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa
kufanya juhudi mbali mbali ikiwemo uanzishwaji wa miradi mikubwa ya maji ili
kuondoa kero kwa wananchi lakini kudumu kwa miradi hiyo kunahitajika kuwepo sera
bora na mipango madhubuti ya kuitunza miradi inayoanzishwa.
Mhe. Othman amesema kwamba
ingawa baadhi ya maeneo bado kuna changamoto ya upatikanaji wa
huduma ya maji lakini ukamilishaji wa mradi huo uliohusisha sheheia za Masingini , Dole na Dimani, Kwarara Kidutani , Mkorogo,
Mfenesini na Maungani itasaidia sana kupunguza changamoto ya huduma hiyo.
Hata hivyo Mhe. Othman amesema
kwamba Zanzibar kumejengeka utamaduni wakuwa wazuri wa kuanzisha miradi ya
maendeleo lakini changamoto kubwa inabaki katika kuitunza na kuendeleza.
Hivyo amekumbusha mamlaka ya maji
na viongozi wanaohusika kuhakikisha kwamba wanapanga na kuweka mikakati bora na
sera imara za matumizi sahihi ya maji ili kupunguza tatizo la matumizi makubwa
yasiyo ya lazima.
Amefahamisha kwamba ni muhimu
katika kuifanya miradi kuwa endelevu kila mmoja miongoni mwa viongozi na
wananchi kutimiza vyema wajibu wao ili wananchi wafaidi huduma zinatokanazo na
fedha zao za kodi kwa miradi inayoanzishwa kuwa na tija zaidi kwao na taifa kwa jumla.
Mhe. Othman amefahamisha kwamba
Zanzibar kunahaja pia kwa viongozi katika ngazi zote ikiwemo halimashauri na
wilaya na mikoa kuhakikisha kwamba wanakuwa na mwelekeo mpya katika mipango ya
kutunza vianzio vya maji nchini ili visiendelee kuharibiwa.
Amesema kwamba eneo la magharibi ya
Zanzibar ndio lenye vianzio muhimu vya
maji lakini sehemu kubwa ya maeneo hayo imekatwa miti na kujengwa nyumba jambo
ambalo litaharibu sio tu mazingira na
kukumbwa na athari za mabadiliko
ya taibia nchi lakini pia na kukosa ama kuharibika vyanzo vya maji.
Amefahamisha kwamba serikali imekuwa
ikiimarisha upatikanaji wa huduma
za maji mijini na vijijini kwa kuendeleza utekelezaji miradi ya maendeleo
ikiwemo uchimbaji wa visima, ulazaji wa mabomba
sambamba na ujenzi wa matangi mapya ya kuhifadhia maji ili kuondoa
changamoto hiyo kwa wananchi hivyo jujudi hizo lazima ziwe sambamba na utunzaji
bora.
Aidha amesema kwa vile ofisi yake
pamoja na mambo mengine lakini inajukumu lakusimamia mazingira hgivi itaanzisha
maradi mkubwa wa kusaidia kuirejesha Zanzibar kuwa ya kijani ambao utahusisha
wanajamii , viongozi wa halamashauri, wilaya na shehia kwa kila mtu kupanda miti na kusaidia
utunzaji wa mazingira.
Amesema paia kunahaja ya kujenga
utamaduni wa kukirithisha kizazi upandaji wa miti ya aina mbali mbali katika
kuhakimkisha utunzaji bora wa mazingira na kuhgifadhi vyema vyanzo vya
upatikanaji wa maji nchini.
Mhe. Othman amesema kwamba
serikali inaishukuru sana ZAWA na
Serikali ya India kupitia Benki yake ya EXIM sambamba na kuipongeza Kampuni ya
Larsen and Toubro Kampuni Elekezi ya
M&S Crux ya Ushauri elekezi kwa kazi nzuri wanaoendelea kuifanya katika
utekelezaji wa mradi huu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa ZAWA Dk .
Salha Mohammed Kasssim, amesema kwamba
mradi huo unatekelezwa kwa Mkopo kutoka EXIM Benk ya India kwa masharti nafuu
ambao unajengwa kwa mashirikiano na wakandarasi watatu na utakapokamilika
utakuwa umekamilisha skimu tatu za maji na jumla ya visima 64 vitachimbwa kwa ajili ya kuondosha tatizo la maji
Zanzibar.
Aidha amesema kwamba kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zitatumiwa na serikali ili
kugharamia ulipaji wa fidia za wananchi ambao mali zao zimeharibiwa kufuatia
maeneo yao kupitiwa na mradi huo ambao
ni mkombozi kwa wazanzibari kwa kuwa utanufaisha idadi kubwa ya wananchi katika shehia mbali mbali zikiwemo kianga ,
dole, mwembe mchomeke,Masingini , mtiufani pamoja na maeneo mengine jirani.
Mapema Mgurugenzi wa mradi huo huo kutoka kampuni ya
L&T kutoka nchini India amesema kwamba utekelezaji wa mradi huo unakwenda
vizuri na upo kwenye hatua kubwa na kuiomba serikali na mamlaka zinazohusika
kuharakikisha utoaji wa vifaa vinavyoingizwa katika utekelezaji wa mradi huo ili
ukamilike kwa wakati.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maaji na Nishati
Ndugu Joseoh Kilangi amesema kwamba uanzishwaji wa mradi huo ni sehemu muhimu
katika utekelezaji wa miradi ya uchumi
wa mbluu ambayo haiwezi kutekelezeka vyema bila maji na umeme kuwa endelevu na
kwamba lazima kuhakikisha kunakuwepomabadiliko katika kutimiza ndoto ya
serikali ya kustawisha huduma kwa wananchi wake.
Mwisho
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa
Kwanza wa Rais Kupitia kitengo chake cha habari leo tarehe 08.01.2022.
No comments:
Post a Comment