Habari za Punde

Singida Big Stars Yaingia Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi 2023

 

Na.Fatawi Ramadhan 

Yanga S C alipaswa kufa Goli 1 _ 0 kama sio Busara ya muamuzi Rashid Farghani "Webu" ambae alifanya maamuzi mabovu ambayo yamewanufaisha Yanga sc kupata Goli la kusawazisha kupitia kwa David Bryson 

Tukio lilivyotokea aliamuru mpira wa kutengwa (In direct freekick) ambao ni faida kwa Yanga sc baada ya kufanyiwa foul Yacouba Asogne tafsiri yake mpira unapaswa kuchezwa na watu 2 kabla ya kuingia wavuni kinyume na hapo hata kama utaingia nyavuni sio Goli 

Ajabu David Bryson alikwenda kupiga mpira ule na kuingia nyavuni bila kuchezwa na Mchezaji mwengine (Direct Freekick) lakini muamuzi akaruhuasu ni Goli jambo ambalo sio sahihi lkn Fouth Official (Muamuzi wa akiba) alimuita na kumkumbusha sheria no 12 ya mchezo wa soka "Fouls and Misconduct" hapo kuna Direct freekick na In_direct freekick  lakini aliweka pamba kwenye masikio na hakutaka kusikia hicho kitu 

Umakini unapaswa kuongezwa hii Michuano ni mikubwa sana wakati huu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Dunia ni kama kiganja sasa hivyo mapenzi yangeekwa pembeni na mwenye haki yake apewe tu (Kila Mtu avune kile alichokipanda) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.