Habari za Punde

DC Moyo Atoa Msaada wa Vyakula kwa Familia 4 Zilizoathirika na Mnyama Tembo

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi msaada kwa wananchi baada kupata athari za mnyama Tembo.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akimkabidhi msaada kwa wananchi baada kupata athari za mnyama Tembo
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe.Mohamed Hassan Moyo akiwasalimia Wanafunzi akiwa katika ziara yake kuwafariji na kutowa msaada wa vyakula kwa familia zilizopata athari kutokana na tembo kuharibu mazao katika mashamba yao katika Kijiji cha Mwandila.

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mohamedi Moyo leo amekabidhi msaada wa chakula jumla ya kilo 120 Kwa familia 4 zilizo hathirika na uvamizi wa Tembo katika kijijij cha Mwandila.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada uwo Dc MOYO ameeleza anafahamu juu ya Changamoto hiyo ya uvamizi wa Tembo katika mashamba na makazi ya wananchi hivyo ameguswa kutoa msaada uwo kwa familia ambazo hazina kabisa,Aidha Moyo ameeleza kuwa serikali inaendelea kuchua atua mbalimbali za kukabiliana na wanyama hao pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata chakula.

Wakizungumza kwa niaba ya familia hizo mwenyekiti wa kijiji hiko Rajabu Chitanda pamoja na diwani wa kata hiyo Ally Milile wamemshukuru mkuu wa wilaya huyo Kwa msaada uwo huku wakiomba serikali kuendelea na jitihada zaidi kwaajili ya kunusulu ari za wananchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.