Katibu wa Baraza La Taifa la Michezo Zanzibar Said Kassim Marine na Katibu wa Uganda Federetion Edgar Mujuni wakiwa katika picha ya paoja baada ya kuzungumza kuhusu kuanzishwa mchezo wa Kabari huko Mwanakwerekwe Miji Zanzibar.
Picha na Miza Othman BTMZ.
Na Miza Othman BTMZ 06/ 2/2023.
Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar limesema lipotayari kushirikiana na mchezo wa Kabari kwani kufanya hivyo kutapelekea kupiga hatua ya kuboresha sekta ya Michezo Zanzibar.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza hilo Said Kassim Marine wakati alipotembelewa na Katibu wa Uganda Kabari Federatin Edgar Mujuni huko Ofisini kwake Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharib “B’” Unguja.
Alisema amemshukuru katibu Edgar Mujuni kwa kuamua makusudi kwa kuja kuendeleza mchezo huo kwani kufanya hivyo kutasaidia kuwainua vijana kujiajiri mchezo wa Kabari hapa Zanzibar.
Hata hivyo alisema baraza la Taifa la Michezo Zanzibar lipo tayari kusajili chama hicho na kutambulishwa kwa lengo la kujua nia na madhumuni ya mchezo wa Kabari hapa Zanzibar.
Nae Katibu wa Uganda Kabari federetion Edgar Mujuni alisema ameamua kuja Zanzibar kuunga na Nchini ya Uganda kupitia mchezo wa Kabari kwa lengo la kuwaboresha Wachezaji wa mchezo huo na kufikia lengo walilokusudia.
Hata hivyo alisema Mchezo huo utasaidia kuleta maendeleo Zanzibar na kuhakikisha matunda yanapatikana kwa kuleta umoja na mashiirikiano ya upigaji hatua ndani ya mchezo huo.
Aidha amelishukuru baraza hilo kwa kumpokea na kuweza kushirikiana na atahakikisha mchezo huo unaleta mafanikio kwani mchezo wa Kabari ni sawa na michezo mengine ikiwemo football na netboll.
Kwa upande wake Katibu wa Zanzibar Kabari Federetion Ahmada Abdalla Ahmada alisema wamefarajika kwa ujio wa katibu huyo watamuunga mkono na kuwa nae bega kwa bega ili kuhakikisha mafanikio ya mchezo huo yanapatikana.
No comments:
Post a Comment