Habari za Punde

Waziri Lela azindua mradi wa Applied Human Intelligence (AHUMAIN)

Mkuu wa Taasisi  ya Sayansi na Teknolojia, ya Karume (KIST), Dkt Mahmoud Abdulwahab Alawi, akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa mradi wa Applied Human Intelligence (AHUMAIN) Kwa upande wa  Afrika Mashariki, huko Ukumbi wa Mkutano wa Dokta Idrissa Muslim Hijja Mbweni Zanzibar,
 Mratibu wa Mradi wa Applied Human Intelligence (AHUMAIN) Ing. Dirk Van Merode akitoa utangulizi wa Mradi huo katika Ukumbi wa Mkutano wa Dokta Idrissa Muslim Hijja Mbweni Zanzibar,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Lela Muhamed Mussa akizindua rasmi mradi wa Applied Human Intelligence (AHUMAIN) Kwa upande wa  Afrika Mashariki, katika Ukumbi wa Mkutano wa Dokta Idrissa Muslim Hijja Mbweni Zanzibar,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Lela Muhamed Mussa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Taasisi  ya Sayansi na Teknolojia, ya Karume (KIST), pamoja na Wadau kutoka Taasisi mbali mbali baada ya  Uzinduzi wa mradi wa Applied Human Intelligence (AHUMAIN) Kwa upande wa  Afrika Mashariki, katika Taasisi ya Karume Mbweni Zanzibar,

                                   Picha na Maryam Kidiko – KIST.

Na Issa mzee - KIST.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Lela Muhamed Mussa, ameisisitiza Taasisi  ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST). kuitumia fursa iliopo katika mraidi wa AHUMAIN ili iweze kuenda sambamba na Teknolojia mpya zinazoibuka Ulimwenguni.

Alisema kutokana na kuibuka kwa Teknolojia mpya mara kwa mara ulimwenguni, ni vyema Taasisi ya Karume ichangamkie fursa za miradi kama hiyo ili iweze kufikia teknolojia ya kisasa, ambapo miongoni mwa njia za kufikia teknolojia hizo ni kuichangamkia fursa iliopo katika mradi wa AHUMAIN utakaowawezesha watanzania kujifunza teknolojia mpya na za kisasa.

Alisema hayo wakati akizindua rasmi mradi wa Applied Human Intelligence (AHUMAIN) Kwa upande wa  Afrika Mashariki, katika Ukumbi wa Mkutano wa Dokta Idrissa Muslim Hijja Mbweni Zanzibar, ambapo kwa Tanzania  Taasisi ya Karume na Chuo kikuu cha Ardhi,  ndio vyuo pekee vilivyo bahatika katika mradi huo .

Alieleza kuwa, kupitia mradi huo wa AHUMAIN Taasisi ya Karume itaweza kuwa na program mbili mpya na za kisasa ikwemo Human Intelligence na Data Science ambazo ni programe muhimu na zenye soko, lakini pia zitasaidia katika kufanikisha maendeleo ya teknolojia Nchini.

Aidha alisema, mradi huo utawawezesha wananchi mbalimbali wa Afrika Mashariki kupata fursa ya kushiriki katika mafunzo mbalimbali yatakayotolewa ndani na nje ya Nchi, hivyo amewataka wananchi kuichangamika fursa hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi  ya Sayansi na Teknolojia, ya Karume (KIST), Dkt Mahmoud Abdulwahab Alawi, amesema mradi wa AHUMAIN ni mradi mwengine ambao umezinduliwa katika Taasisi ya Karume, uliolenga  katika kuhakikisha Zanzibar na Tanzania kwa ujumla inakwenda sambamba na Teknolojia mpya ambazo zinaibuka katika mataifa ili maendeleo ya teknolojia yaweze kupataika kwa haraka.

 Alisema kuwa, maendeleo ya Viwanda na Teknolojia kwa ujumla, yanazidi kukua Duniani, hivyo ni lazima nchi za afrika zitafute fursa ya kuweza kupata maendeleo ya teknolojia, ikiwemo kushiriki katika miradi kama hii inayojumuisha Taasisi mbalimbali ulimwenguni.

Aidha alitumia fursa hiyo kuupongeza Umoja wa Ulaya pamoja na Vyuo Vikuu mbalimbali duniani,  kwa kutoa ushirikiano wa karibu na Taasisi ya Karume katika mradi huo wenye faida kubwa kwa Taasisi na Tanzania kwa ujumla.

Akitoa ufafanuzi kuhusu mradi huo, Mratibu wa Mradi huo Katika Taasisi ya Karume, Mkufunzi Ali Abdullah, amesema mradi huo unalenga kuipa uwezo kompyuta kufanya maamuzi ya kibinaadamu yaliyosahihi na yaharaka, ili kufanikisha kazi kwa wakati  na kuongeza uzalishaji wa bidhaa hasa viwandani.

Alisema mataifa yaliyoendelea yanapiga hatua kubwa katika maendeleo, kutokana na matumizi ya teknolojia za kisasa, hivyo ipo haja kwa Nchi za Afrika kuitumia fursa hiyo kwa lengo la kukuza uzalishaji.

Kikao hicho kilishirikisha wadau mbalimbali kutoka Taasisi za Afrika mashariki na Vyuo Vikuu vya mataifa mbalimbali ya Ulaya.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.