Habari za Punde

Wiki ya Kumlinda Mtumiaji Zanzibar

Afisa uhusiano Tume ya Ushindani halali wa Biashara Zanzibar (ZFCC) Ibrahim Hamad Makame akiwaonyesha Waandishi wa Habari mfano wa Bidhaa iliyokopiwa wakati alipokua akiwapatia elimu kuhusiana na  haki za mtumiaji katika shamrashamra  za wiki  ya kumlinda mtumiaji zilizofanyika Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi  Kisonge ,na kufikiwa kilele chake  tarehe 15 mwezi huu Jijini Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala

Afisa mwana sheria wa Baraza la Ushindani halali wa Biashara Zanzibar (ZFCT) Mgeni Abdulla Mohammed akitoa maelezo kuhusiana na Baraza hilo  wakati alipotembelewa na Waandishi wa Habari huko Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi  Kisonge,ikiwa ni shamrashamra za kuadhimishi wiki ya kumlinda mtumiaji, na kufikiwa kilele chake  tarehe 15 mwezi huu Jijini Mwanza yakiwa na kauli mbiu “kumjengea uwezo mtumiaji katika matumizi ya nishati na nishati mbadala” .PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO ZANZIBAR. 14.03.2023

Na Rahma Khamis,Maelezo                                               

Wananchi wametakiwa kuchukua risiti zao wakati wanapokwenda kupeleka malalamiko katika baraza la Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar (ZFCT)  ili kuepuka usumbufu wakati wa kutatuliwa malalamiko yao .

 

Wito huo umetolewa  na Afisa Mwanasheria wa hilo  Mgeni Abdulla Mohammed katika Uwanja wa Mnara wa kumbukumbu Kisonge  wakati alipokua Akitoa elimu kwa wananchi kuhusu haki ya mtumiaji katika bidhaa ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kumlinda mtumiaji. 

 

Amesema risiti ni jambo muhimu kwa mlalamikaji kutokana na kuwa ni ushahidi tosha utakaomuongoza mtoa maamuzi katika kulitafutiwa ufumbuzi lalamiko alilofikishiwa na mtumiaji.

 

Aidha Mwanasheria amesema kila mtu ni mtumiaji  wa bidhaa katika jamii hivyo ni wajibu wao kufahamu haki na wajibu wao ili kuepuka matatatizo yanayoweza kujitokeza.

 

"Watu wote ni watumiaji kama hatujatumia Mchele tunanunua bidhaa nyengne au tunapanda usafiri hivyo ni wajibu wetu kujua haki zetu katika kutumia bidhaa ili malalamiko yanayoweza kuepukika .” alisema Mwanasheria.

 

Hata hivyo Mwanasheria huyo amewasisitiza wananchi kuangalia bidha zao wanaponunua kabla ya matumizi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitikeza .

 

Nae Afisa Uhusiano wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Ibrahim Hamad Makame amesema mtumiaji ana haki ya kulindwa dhidi ya bidhaa na huduma zisizo salama ambazo zinaweza kuangamiza Mali na kuhatarisha Afya ya mtumiaji.

 

Aidha amefahamisha kuwa mbali na kutambua haki yake pia ana  haki ya kupata maelezo sahihi kuhusu bei,ujazo na malighafi zinazounda bidhaa zitakazomuezesha kufanya maamuzi ya kununua bidhaa sahihi.

 

Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa wamefarajika kupatiwa elimu hiyo kwani walikua hawfahamu chochote kuhusu haki za mtumiaji wa bidhaa.

 

Kilele cha Maashimisho ya wiki ya kumlinda mtumiaji yanatarajiwa kufanyika kesho Jijini Mwanza ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu “KUMJENGEA UWEZO MTUMIAJI KATIKA MSTUMIZI YA NISHATI NANISHATI MBADALA.”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.